• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 21, 2013

  YANGA SC WAPANGWA KUNDI C LAINI KAGAME, SIMBA KUNDI A LA HATARI TUPU

  Mabingwa watetezi; Yanga SC wamepangwa Kundi C

  Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 21, 2013
  SAA 4:00 USIKU
  BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limewapanga katika Kundi C, mabingwa watetezi, Yanga SC katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati, Kombe la Kagame leo katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 18 hadi Julai 2, mwaka huu mjini Khartoum, Sudan.
  Katika kundi hilo, mabingwa hao mara mbili mfululizo wa taji hilo wamepangwa na Ports ya Djibouti, Express ya Uganda na  Vital 'O'  ya Burundi, wakati wapinzani wao wa jadi, Simba SC wamepangwa kundi A pamoja na wenyeji El-Mereikh, Elman  ya Somalia na APR ya Rwanda
  Mabingwa wa Kenya, Tusker wamepangwa Kundi B pamoja na wenyeji wengine, Al-Hilal, Al Ahly Shandy ya Sudan, Falcons ya Zanzibar na Al-Nasir Juba ya Sudan Kusini.
  Yanga itaanza kampeni zake Juni 20 kwa kumenyana na Express na Simba SC itashuka dimbani Juni 21 kufungua dimba na El-Mereikh, mechi zote zikichezwa Elfashar.
  Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye amesema zawadi za washindi zimeongezeka kutoka dola za Kimarekani 60,000 anazotoa Rais wa Rwanda, Paul Kagame hadi dola 80,000 baada ya Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji kuongeza dola 20,000.
  Lakini Musonye amesema wanataka zawadi za washindi ziwe jumla dola 100,000 hivyo wanatafuta fedha za kuongezea. 
  Wawakilishi; Simba SC wapo Kundi A la kifo


  KUNDI A: El-Merrekh -(Sudan), APR (Rwanda), 
  Simba SC (Tanzania), Elman (Somalia) - EL FASHER
  KUNDI B: Al-Hillal (Sudan), Tusker (Kenya), Al Nasri (Sudan Kusini), Falcon (Zanzibar),  Al Shandy (Sudan) - KADUGLI
  KUNDI C: Yanga SC (Tanzania), Express (Uganda), Ports (Djibout), Vitaloo (Burundi) - EL FASHIR

  RATIBA KOMBE LA KAGAME KUANZIA JUNI 18 HADI JULAI 2, 2013 (EL-FASHIR NA KADUGLI - SUDAN)
  TAREHETIMUTIMUKUNDI/MUDAUWANJA
  18.06.2013.TUSKER SUPER FALCON B - SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
  AL HILLAL AL NASRI B -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
  19.06.2013.VITALOOPORTS  C - SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
  20.06.2013.YANGA SC EXPRESS C - SAA 8:00 MCHANAEL-FASHER
  20.06.2013.ELMAN FC APR FC A - SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
  20.06.2013.SUPER FALCON AL NASRI B -SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
  20.06.2013.TUSKER AL-SHANDY B -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
  21.06.2013.EL MERREIKH SIMBA SC A -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
  22.06.2013.EXPRESS FC VITALOO C - SAA 8:00 MCHANAEL-FASHER
  PORTS YANGA SC C -SAA 10:00 JIONIEL FASHER
  22.06.2013.AL NASRITUSKER B - SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
  AL SHANDY AL HILAL B -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
  23.06.2013APR SIMBA SC A - SAA 8:00 MCHANAEL-FASHER
  EL MERREIKH  ELAM FC A -SAA 10:00 JIONI
  EL-FASHER
  24.06.2013AL NASRI AL SHANDY B -SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
  SUPER FALCON AL HILLAL B -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
  24.06.2013. PORTSEXPRESS FC C -SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
  25.06.2013.VITALOO YANGA SC C -SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
  26.06.2013.AL SHANDY SUPER FALCON B -SAA 8:00 MCHANAKADUGLI
  AL HILLAL TUSKER B -SAA 10:00 JIONIKADUGLI
  26.06.2012.SIMBA SC ELMAN FC A -SAA 8:00 MCHANAEL-FASHER
  APR FC EL MERREIK A -SAA 10:00 JIONIEL-FASHER
  27.06.2013.MAPUMZIKOMAPUMZIKOMAPUMZIKO
    MAPUMZIKO
  28.06.2013.(23) B2 VS C2(24) B1 VS BEST QUTATANGAZWAKADUGLI
  28.06.2013.(25) C1 VS A2(26) A1 VS B3UTATANGAZWAEL-FASHER
  30.06.2013.WNR 23 VS WNR 25WIN 24 VS WIN 26UTATANGAZWA
  01.07.2013.MAPUMZIKOMAPUMZIKOMAPUMZIKOMAPUMZIKO
  02.07.2013.ILIYOFUNGWAILIYOFUNGWAMSINDI WA TATUEL-FASHER
   ALIYESHINDA 27 ALIYESHINDA 28  FAINALI EL-FASHER
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: YANGA SC WAPANGWA KUNDI C LAINI KAGAME, SIMBA KUNDI A LA HATARI TUPU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top