• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 21, 2013

  BENITEZ KUTUA PSG KURITHI MIKOBA YA ANCELOTTI ANAYEKWENDA KUCHUKUA NAFASI YA MOURINHO REAL MADRID ANAYEREJEA CHELSEA


  IMEWEKWA MEI 21, 2013 SAA 1:15 USIKU
  KOCHA wa muda wa Chelsea ya England, Rafa Benitez ameombwa na klabu ya Paris Saint German ya Ufaransa kuifundisha timu hiyo, kwa mujibu wa gazeti la L'Equipe. 
  Benitez ataiongoza Chelsea katika mechi zake mbili za mwisho dhidi ya Manchester City Marekani na baada ya hapo atakuwa huru.
  Wanted man: PSG have put Rafa Benitez on their shortlist
  Anayetakiwa: PSG inamtaka Rafa Benitez

  Huku Carlo Ancelotti akiwa mbioni kuhama PSG kwenda kurithi mikoba ya Jose Mourinho, Real Madrid - na Special One akitarajiwa kufanya urejeo maalum Stamford Bridge - Benitez anaweza kuwa mtu sahihi kurithi viatu vya Ancelotti pale PSG. 
  Benitez ametwaa taji la Europa League na kuiwezesha The Blues kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, lakini hajaweza kuwashawishi mashabiki kumkubali tangu arithi mikoba ya Roberto di Matteo aliyefukuzwa. 
  On his way: Carlo Ancelotti is set to take over at Real Madrid in the summer
  Yuko njiani: Carlo Ancelotti anajiandaa kutimkia Real Madrid

  Gazeti hilo la Ufaransa, L'Equipe limesema klabu tayari imemuomba Benitez kuchukua nafasi na Mspanyola huyo na ameonyesha yu tayari kujiunga na Matajiri hao wa Ufaransa.
  Wakala wa Benitez pia bado hajakaa ofa ya mteja wake kutoka Napoli ya Italia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BENITEZ KUTUA PSG KURITHI MIKOBA YA ANCELOTTI ANAYEKWENDA KUCHUKUA NAFASI YA MOURINHO REAL MADRID ANAYEREJEA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top