• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 28, 2013

  TOURE AFAULU VIPIMO KUJIUNGA NA LIVERPOOL


  IMEWEKWA MEI 28, 2013 SAA 4:54 USIKU
  BEKI Kolo Toure atakuwa rasmi mchezaji wa Liverpool ifikapo Julai 1, baada ya kukamilisha vipimo vya afya katika harakati zake za kuhamia Anfield.
  Liverpool imekubali kumpa mkataba wa miaka miwili ambao utamfanya ashuke kiwango cha mshahara ch Pauni 90,000 kwa wiki alizokuwa akilipwa Manchester City. 
  Mkataba wake unamalizika Juni 30 na taratibu za uhamisho wake kama mchezaji huru zitafuatia baada ya hapo.
  To the rescue: Kolo Toure is set to complete his move to Liverpool from Manchester City
  Brendan Rodgers anajaribu kuimarisha safu ya ulinzi ya Liverpool baada ya kuondoka kwa Jamie Carragher aliyestaafu na wakati Toure haendani na vigezo vya kusajiliwa timu hiyo chini ya Fenway Sports Group, beki huyo mwenye umri wa miaka 32 anabebwa na uzoefu wake.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: TOURE AFAULU VIPIMO KUJIUNGA NA LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top