• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 31, 2013

  AZAM YASAJILI WATATU WAKIWEMO WAWILI WA UJERUMANI...NI MAKINDA TUPU

  Amepandishwa; Mudathir Yahya
  Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA MEI 31, 2013 SAA 5:25 ASUBUHI
  WAKATI Simba na Yanga SC zinakwenda mbio kusajili wachezaji wapya, washindi wa pili mara mbili mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC wao wamesema hawasajili hata mchezaji mmoja, zaidi watapandisha wachezaji kutoka katika akademi yao.
  Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa ameiambia BIN ZUIBEIRY leo asubuhi kwamba, kocha Muingereza Stewart Hall amesema kwa sasa hakuna umuhimu wa kusajili, zaidi ya kuiangalia timu kwanza katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, unaotarajiwa kuanza Agosti.
  Nassor amesema kwamba kocha amewaambia iwapo atagundua kuna mapungufu katika timu katika kipindi cha kuanzia Agosti, ndipo atasajili Novemba katika dirisha dogo.
  “Unajua mwakani ndio tutakuwa na haya mashindano ya Afrika (Kombe la Shirikisho). Na pia ndio mbio za ubingwa wa Ligi Kuu (Bara) zinapamba moto. Kwa hiyo mwalimu ameomba hicho ndicho kipindi kizuri kusajili,”alisema.
  Hata hivyo, Nassor alisema kwamba kocha amependekeza wachezaji kadhaa wasajiliwe kutoka katika akademi ya klabu hiyo, wakiwemo Mudathir Yahya ambaye yupo na timu ya taifa Ethiopia, kipa Hamad Kadebi na Dissmas ambaye kwa sasa yuko kwenye majaribio Ujerumani.
  “Tuna vijana wengi wazuri katika akademi yetu, mwalimu anawapa nafasi sasa. Anaamini timu yake ipo vizuri na hana haja ya kuhangaika kutafuta wachezaji wapya,”alisema Nassor.
  Mudathir pia alikuwa kwenye majaribio nchini Ujerumani, akarudishwa nchini kujiunga na timu ya taifa, Taifa Stars kujiandaa kwa mchezo wa kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Ethiopia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: AZAM YASAJILI WATATU WAKIWEMO WAWILI WA UJERUMANI...NI MAKINDA TUPU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top