• HABARI MPYA

  Jumatano, Mei 29, 2013

  BENITEZ AZIFANYA KITU MBAYA CHELSEA NA MAN CITY...BAADA YA KUTUA NAPOLI, AWEKA NGUMU CAVANI KUONDOKA

  IMEWEKWA MEI 29, 2013 SAA 1:02 USIKU
  KOCHA mpya wa Napoli, Rafa Benitez anataka kumzuia kuondoka katika klabu hiyo mshambuliaji, Edinson Cavani na atafanya naye mazungumzo mshambuliaji wake nyota huyo kumshawishi abaki kwa mmoja zaidi. 
  Cavani, mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akiwaniwa kwa muda mrefu na Manchester City na ameingia kwenye orodha ya washambuliaji tishio Ulaya kwa kuweza kufunga mabao 29 katika mechi 34 za ligi akiwa na Napoli.
  Chelsea pia inamtaka mchezaji huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni 50 na anayetaka mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki.
  In demand: After scoring 29 goals in 34 games for Napoli this season, Cavani (right) is the subject of interest from Chelsea and Manchester City
  Anatakiwa: Baada ya kufunga mabao 29 katika mechi 34 akiwa Napoli msimu huu, Cavani (kulia) sasa anazivutia Chelsea na Manchester City

  Wiki iliyopita, Napoli iliikata maini City katika mpango wa kumtaka Cavani, kwa kuwapa ofa ya Pauni Milioni 60 kwa ajili ya Edin Dzeko.
  Rais wa klabu hiyo ya Italia, Aurelio De Laurentiis, ambaye alikuwa hataki kuizungumzia City awali, alisafiri hadi London Jumatatu kufanya mazungumzo Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo ya Ligi Kuu England, Riccardo Bigon.
  City iko tayari kukubali Pauni Milioni 50 – kati ya hizo, Pauni Milioni 30 ni thamani ya Dzeko na kuongeza Pauni Milioni 20– lakini Napoli inataka Milioni 60 na De Laurentiis anasema ni wakati wa kumalizana au kuacha.
  Benitez alitangazwa kuwa kocha mpya Napoli Jumatatu akipewa mkataba wa miaka miwili. Mspanyola huyo anachukua nafasi ya Walter Mazzarri ambaye anahamia Inter Milan, klabu ya zamani wa Benitez.
  VIDEO: Angalia mabao ya Cavani Serie A msimu wa 2012-13
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BENITEZ AZIFANYA KITU MBAYA CHELSEA NA MAN CITY...BAADA YA KUTUA NAPOLI, AWEKA NGUMU CAVANI KUONDOKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top