• HABARI MPYA

    Monday, May 20, 2013

    MISS TANGA JAMANI KUMEKUCHA, HAO VIMWANA TEMEA MATE CHINI...

    Theresia Kimaro, Miss Tanga mwaka jana

    Na Princess Asia, IMEWEKWA MEI 20, 2013 SAA 11:05 JIONI
    SHINDANO la kumtafuta malkia wa Mkoa wa Tanga mwaka huu, Redd's Miss Tanga 2013 limepangwa kufanyika Juni 22, kwenye Uwanja wa Mkwakwani, mkoani humo.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo Mkurugezi wa 
    Kampuni ya DATK Entertainment, Asha Kigundula, alisema kwamba warembo tayari wameanza mazoezi kwenye Ukumbi wa Lavida uliopo jijini Tanga.
    Asha, amesema shindano hilo litaanza saa 2:00, usiku, ikiwa ni pamoja na kuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa moja ya bendi maarufu hapa nchini, pamoja na wasanii wanaotamba katika muziki wa kizazi kipya.
    Amesema maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri jumla ya warembo 14 watashindania taji hilo na kwamba hadi juzi warembo 10 walikuwa wamekwishajitokeza mazoezini, chini ya walimu, Theresia Kimaro na Mwanaidi Omar.
    Warembo hao na umri wa kwenye mabano ni Hawa Ramadhani (18), Hazina Mbaga (19), Like Abdulrahman (19), Jacque Emannuel (18), Wahida Mmbwambo(20), Tatu Hussein(19), Mwana Hamisi Mashaka (20), Neema Abdallah (18), Lulu Mbonea (19) na Aisha Rashid (21).
    “Kila kitu kinaendelea vizuri, ikiwa na warembo 
    kuendelea kujiandikisha kushiriki shindano la mwaka huu, ambalo nina hakika litakuwa la aina yake"amesema Asha.
    Redd's Miss Tanga 2013, imedhaminiwa na BIN ZUBEIRY Blog, CXC Africa, Executive Solutions, Busta General Supply, Mkwabi Enterprises, Lusindic Investment LTD, Lavida Pub, Jambo Leo, Staa Spoti, Five Brothers, Cloud's Media Group, Michuzi Media Group, Saluti5, Kajuna, JaneJohn na Kidevu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MISS TANGA JAMANI KUMEKUCHA, HAO VIMWANA TEMEA MATE CHINI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top