• HABARI MPYA

  Jumamosi, Mei 25, 2013

  TIMU YA KALI ONGALA YAKIPIGA LIGI YA MABINGWA

  Kali Ongala aliibukia Abajalo

  Na Boniface Wambura, IMEWEKWA MEI 25, 2013 SAA 5:00 USIKU
  RAUNDI ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inaendelea kesho (Mei 26 mwaka huu) kwa mechi sita za kwanza zitakazochezwa katika miji sita tofauti.
  Abajalo ya Sinza, Dar es Salaam iliyomuinua Kocha Msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala akasajiliwa Yanga SC mwaka 1999 kabla ya kwenda kucheza soka ya kulipwa Amerika na Ulaya, itamenyana na na Kariakoo ya Lindi kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam wakati Machava FC ya Kilimanjaro itakuwa mwenyeji wa Mpwapwa Stars ya Dodoma kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
  Nayo Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida huku Polisi Jamii ya Bunda mkoani Mara ikimenyana na Biharamulo FC ya Kagera kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
  Mjini Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika ni kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi Warriors ya Katavi wakati Njombe Mji itaikaribisha Kimondo SC ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
  Leo (Mei 25 mwaka huu) Friends Rangers ya Kinondoni, Dar es Salaam inacheza na African Sports ya Tanga kwenye Uwanja wa Azam Chamazi. Mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.
  Timu zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: TIMU YA KALI ONGALA YAKIPIGA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top