• HABARI MPYA

  Jumatano, Mei 22, 2013

  RAIS REAL MADRID AMPELEKA RONALDO CHELSEA BADALA YA MAN UNITED...NA ASEMA...


  IMEWEKWA MEI 22, 2013 SAA 5:00 USIKU
  RAIS wa zamani wa Real Madrid, Ramon Calderon amekuza matumaini ya Cristiano Ronaldo kufuatana na Jose Mourinho Chelsea... baada ya kupuuza nafasi ya Manchester United kumsajili tena nyota huyo Mreno.
  Ronaldo, mwenye umri wa miaka 27, yuko kwenye kinyang'anyiro cha kununuliwa kwa Pauni Milioni 80, baada ya kuchoshwa na maisha katika Jiji la Hispania.
  Alipoulizwa kama 'kipepeo' huyo wa Ureno alikuwa ana furaha Real Madrid, Calderon alisema: "Ronaldo amesema alikuwa ana machungu mwanzoni mwa msimu. Nafikiri uhusiano wake na rais wa sasa si mzuri, labda kwa sababu rais hapendi wachezaji aliowakuta.
  Wanted: Mourinho hopes to bring Ronaldo with him from Real Madrid to Chelsea this summer
  Anayetakiwa: Mourinho anatumai kuondoka na Ronaldo Real Madrid kuhamia naye Chelsea msimu ujao
  One of the best: Ronaldo scored his 55th goal of the season for Real Madrid last night
  Mmoja kati ya bora: Ronaldo amefunga mabao 55 msimu huu Real Madrid

  "Si timu nyingi zinazoweza kumlipa kile anachostahili na pia itakayoweza kuilipa Real Madrid kile wanachotaka. Kuna klabu tatu - Manchester City, PSG na Chelsea. Sifikiri klabu yoyote nyingine inaweza kulipa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya mchezaji.
  "Wao (Real) wanakwenda kujadili mkataba sasa na watafanya uamuzi. Ni kitu ambacho kitajulikabna ndani ya wiki chache,"alisema.
  United ina nafasi ya kwanza ya kumsajili Ronaldo ikiwa Real itaamua kumuuza nyota huyo wa Ureno itampa kipaumbele cha kurejea Old Trafford. 
  Lakini Mourinho, ambaye amefanya naye kazi kwa miaka mitatu iliyopita Bernabeu, amemuweka kwenye orodha ya wachezaji anaowataka kwa ajili ya timu yake mpya.
  Wayne Rooney wa Manchester United, ambaye angependa kuhamia Chelsea, na mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani pia wanatakiwa na Mourinho.
  On the list: Manchester United's Wayne Rooney is also wanted by Mourinho
  On the list: Napoli's Edinson Cavani is also wanted by Mourinho
  Wamo kwenye orodha: Wayne Rooney (kushoto) na Edinson Cavani pia wanatakiwa na Mourinho
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: RAIS REAL MADRID AMPELEKA RONALDO CHELSEA BADALA YA MAN UNITED...NA ASEMA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top