• HABARI MPYA

    Friday, May 24, 2013

    BINGWA EUROPA LEAGUE KUFUZU MOJA KWA MOJA LIGI YA MABINGWA


    IMEWEKWA MEI 24, 2013 SAA 2:00 USIKU
    BINGWA wa Europa League atafuzu moja kwa moja kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kuanzia msimu wa 2015-16.
    Mpango huo wa UEFA umelenga kuyapatia umaarufu mashindano yake hayo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu, ambayo Chelsea ilitwaa taji lake mapema mwezi huu. 
    Inafahamika kwamba, bingwa wa Europa League na Ligi ya Mabingwa hawawezi kucheza michuano hiyo iwapo watakosa nafasi kupitia ligi za nchini mwao.
    Chelsea ilitwaa taji baada ya kuifunga Benfica kwa bao la dakika za lala salama la Branislav Ivanovic lililotengeneza ushindi wa 2-1 dhidi ya klabu hiyo ya Ureno.
    Up for the cup: Chelsea celebrate winning this year's Europa League after a 2-1 victory over Benfica
    Chelsea wakishangilia taji lao la Europa League baada ya kuifunga 2-1 Benfica.

    MABINGWA WA EUROPA LEAGUE 
    (Waliowekewa * hawakufuzu Ligi ya Mabingwa) 

    MWAKABINGWA 
    2013Chelsea
    2012Atletico Madrid*
    2011Porto
    2010Atletico Madrid*
    2009Shakhtar Donetsk*
    2008Zenit St Petersburg
    2007Sevilla
    2006Sevilla*
    2005CSKA Moscow*
    2004Valencia
    Zote Chelsea na Benfica zilitolewa katika Ligi ya Mabingwa  na kushindwa kuvuka hatua ya makundi.
    Sheria mpya itamaanisha England inaweza kuwa na timu tano katika Ligi ya Mabingwa msimu wa 2015-16 kama moja ya klabu zake itabeba taji la Europa League mwaka 2015 na kumaliza nje ya Nne Bora katika Ligi Kuu.
    Wigan, Swansea na Tottenham wataiwakilisha England katika Europa League msimu ujao.
    Wakati huo huo, UEFA imepitisha adhabu ya mechi 10 kwa mechi za Ulaya, iwapo mchezaji au kiongozi anakutwa na hatua ya ubaguzi. 
    Ubaguzi wa mshabiki utaiponza timu kucheza na mashabiki wachache kwa hatua ya kwanza ya usalama na kufungwa kwa Uwanja mzima kwa hatua ya pili ya usalama.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BINGWA EUROPA LEAGUE KUFUZU MOJA KWA MOJA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top