• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 21, 2013

  MOURINHO SASA HURU KUREJEA CHELSEA BAADA YA KUFUKUZWA 'KISTAARABU' REAL MADRID


  IMEWEKWA MEI 21, 2013 SAA 12:30 ASUBUHI
  KAMA amefukuzwa. Kocha Jose Mourinho yuko huru kurejea Chelsea, baada ya rais wa Real Madrid, Florentino Perez juzi usiku kusitisha malipo Pauni 12 za kuvunja mkataba wake.
  Perez ametangaza kwamba, matatizo ya Mourinho miaka yake mitatu kazini Bernabeu vitaisha mwezi ujao, baada ya kufanya mazungumzo na kocha huyo Mreno mwishoni mwa wiki.
  Mourinho ana miaka minne katika mkataba wake bado. Ataiongoza timu Jumapili dhidi ya Real Sociedad na kisha katika mechi ya nyumbani dhidi ya Osasuna, Juni 1.
  Special gone: Jose Mourinho has been sacked as Real Madrid manager, with a return to Chelsea on the cards
  Special anaondoka: Jose Mourinho amefukuzwa ukocha wa Real Madrid na sasa yuko kurejea Chelsea
  Mourinho
  Early bath: Mourinho was sent off in Real's 2-1 Copa Del Rey final defeat by Atletico
  Kitimutimu: Mourinho alitolewa nje kwa kadi nyekundu Real ikilala 2-1 katika Fainali ya Copa Del Rey dhidi ya Atletico

  Perez, mwenye matumaini ya kumtwaa kocha wa Paris Saint-Germain, Carlo Ancelotti, alisema: "Klabu na kocha tumekubaliana ni wakati mwafaka kumaliza uhusiano wetu. Tungependa kumshukuru Jose kwa kazi yote ngumu. Timu imeimarika katika miaka yake mitatu na tunamtakia kila la heri.’
  Special One ataondoka rasmi katika nafasi yake Bernabeu Juni 3 na Chelsea inatumai kumtambulisha katika Mkutano na Waandishi wa Habari Stamford Bridge wiki inayofuata.
  Taking his place: PSG boss Carlo Ancelotti is lined up to be the man to step into Mourinho's shoes
  Anachukua nafasi: Kocha wa PSG, Carlo Ancelotti anatarajiwa kuvaa viatu vya Mourinho
  Come home: Mourinho's return to Chelsea would be a popular move among the Stamford Bridge crowd
  Njoo nyumbani: Kurejea kwa Mourinho Chelsea kutakuwa jambo kubwa na zuri mbele ya umati wa Stamford Bridge

  Stat attack: Mourinho has the best win percentage in Premier League history
  REKODI: Mourinho ana rekodi nzuri zaidi ya ushindi katika Ligi Kuu England kihistoria
  Perez alisema: "Tumepiga hatua kubwa katika maana ya ushindani. Sasa tunarejea tulipokuwa. Kabla, tuliondoledwa Ligi ya Mabingwa katika hatua ya 16 Bora tu na sasa tunaingia kwenye makundi wakati wote.
  "Tumecheza soka ya nguvu msimu uliopita. Tumetikisa dunia kwa kufika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa na Fainali ya Copa del Rey, itakuwa inatosha kwetu, lakini haitoshi,"alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MOURINHO SASA HURU KUREJEA CHELSEA BAADA YA KUFUKUZWA 'KISTAARABU' REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top