• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 21, 2013

  LIUNDA KUTATHMINI WAAMUZI MECHI YA FIFA

  Ulaji FIFA; Leslie Liunda ameula

  Na Mwandishi Wetu, IMEWEKWA MEI 21, 2013 SAA 8:20 MCHANA
  SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limemteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa mtathmini wa waamuzi (referee assessor) katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia.
  Mechi hiyo ya Kundi B, Kanda ya Afrika kati ya Cape Verde na Equatorial Guinea itafanyika Juni 8 mwaka huu saa 10.30 jioni kwenye Uwanja wa Verzea mjini Praia.
  Waamuzi wa mechi hiyo ambao watatoka Angola ni Martins De Carvalho Helder, Dos Santos Jerson Emiliano, Da Silva Lemos Julio na Muachihuissa Caxala Antonio. Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Diarra Massa Momoye wa Mauritania.
  Waamuzi hao, ndiyo waliochezesha mechi ya Kundi D, kati ya Tanzania na Morocco mjini Dar es Salaam miezi miwili iliyopita na Taifa Stars ikashinda mabao 3-0, ukiondoa Kamisaa Diarra pekee. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: LIUNDA KUTATHMINI WAAMUZI MECHI YA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top