• HABARI MPYA

    Friday, May 31, 2013

    REAL MADRID YATOA PAUNI MILIONI 40 KUMNASA SUAREZ...LIVERPOOL YAWAKA KINOMA

    IMEWEKWA MEI 31, 2013 SAA 2:00 ASUBUHI
    MSHAMBULIAJI Luis Suarez inaonekana yuko njiani kuondoka Anfield baada ya jana usiku, kuibuka madai kwamba Real Madrid imetoa ofa ya Pauni Milioni 40 kumhamishia Bernabeu.
    Kiasi cha saa 24 baada ya mpachika mabao huyo wa Liverpool kuiambia Redio ya Uruguay itamuwia vigumu kuwakatalia Madrid wakimtaka, gazeti maarufu Hispania, Marca limeripoti kwamba makubaliano yamefikiwa kumfanya awe mchezaji wa Real. 
    Strike: Suarez scored 23 league goals in 33 appearances for Liverpool last season
    Liverpool wamekasirishwa na habari za kwamba Real imeanza mchakato wa kumsajili Suarez bila kuwasiliana na klabu ya mchezaji huyo. Imesema Suarez atakuwa amekiuka mkataba wake kufanya mazungumzo na Real bila ridhaa ya klabu.
    Suarez pia amewaruka Marca juu ya taarifa yao, ingawa bado mustakabali wake Anfield uko shakani. "Si kweli nina makubaliano na Real Madrid. Nafikiria mustakabali wangu, lakini bado sijaamua chochote,"alisema’ 
    Rais wa Real, Florentino Perez amemzungumzia mchezaji huyo na kusema: "Suarez ni mchezaji mkubwa, na nina uhakika klabu zote duniani zinamtaka. Nampenda,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: REAL MADRID YATOA PAUNI MILIONI 40 KUMNASA SUAREZ...LIVERPOOL YAWAKA KINOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top