• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 28, 2013

  KIMENUKAAA; RAIS REAL MADRID AAHIDI KUMPA CHOCHOTE RONALDO ILI MRADI ABAKI BERNABEU...KWANZA, ATAMFANYA CRISTIANO AWE MCHEZAJI ANAYELIPWA ZAIDI DUNIANI


  IMEWEKWA MEI 28, 2013 SAA 11:00 JIONI
  RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez anajiandaa kumfanya Cristiano Ronaldo awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani katika jithada za kumshawishi abaki Bernabeu, baada ya kuondoka kwa Jose Mourinho.
  Perez amesema: "Ningependa Cristiano Ronaldo awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani. Tunakwenda kufanya kila kitu katika mikono yetu kumfanya awe na furaha.’
  Nyota huyo wa zamani wa Manchester United amekuwa akihusishwa na uvumi wa kurejea Old Trafford msimu ujao au kwenda kujiunga na Matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain - lakini Perez anapambana kumzuia Madrid kwa muda zaidi. 
  Bumper deal: Perez is prepared to break the bank to keep Ronaldo at Real
  Dili kweli: Perez anajiandaa kubomoa benki ili Ronaldo abaki Real
  Star man: Ronaldo had another fine season despite Real not winning a major trophy
  Nyota kweli: Ronaldo alikuwa na msimu mwingine mzuri Real licha ya kutoshinda taji lolote
  Unhappy: Ronaldo is thought be considering a move away from the Spanish capital
  Hana furaha: Ronaldo inasadikiwa anataka kuondoka Hispania

  Ronaldo amekuwa mchezaji mkubwa duniani tangu anunuliwe kwa Pauni Milioni 80 kutua Hispania mwaka 2009, akifunga mabao 146 katika mechi 135.
  Rais wa Madrid pia amesema kwamba licha ya matatizo yote yaliyotokea na Special One msimu huu, wachezaji bao wanamzungumzia vizuri Mourinho.
  Alisema: "Wachezaji wanamzungumzia vizuri tu Mourinho. Wameniambia alikuwa bora. Hatujui nani atakuwa kocha mpya. Tutazungumzia hilo wiki ijayo. Lakini tunataka Zinedine Zidane awe kiongozi wa mpango huu,"alisema.
  Kazi ya kwanza ya Zidane ni kuhakikisha anamsajili nyota wa Tottenham, Gareth Bale kwa Pauni Milioni 65.
  Power-brokers: Perez (above) and Zidane (below) want to unite Ronaldo and Bale at the Bernabeu
  Rais wa Real, Perez anataka Ronaldo abaki na Bale atue Bernabeu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: KIMENUKAAA; RAIS REAL MADRID AAHIDI KUMPA CHOCHOTE RONALDO ILI MRADI ABAKI BERNABEU...KWANZA, ATAMFANYA CRISTIANO AWE MCHEZAJI ANAYELIPWA ZAIDI DUNIANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top