• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 28, 2013

  UBAKHILI WA ARSENAL HATARINI KUWAKOSESHA BONGE LA KIFAA CHA SERIE A


  IMEWEKWA MEI 28, 2013 SAA 11:08 ALFAJIRI
  MPANGO wa Arsenal kumsajili Stevan Jovetic uko hatarini kubuma kwa sababu zile zile mashuhuri za klabu hiyo ya London, 'ubakhili uliotukuka'.
  Arsenal imeshindwa kutoa dau la Pauni Milioni 25 ambalo Fiorentina wanataka ili kumtoa Jovetic.
  Mazungumzo baina ya klabu hizo mbili yamekuwa yakiendelea kwa wiki kadhaa sasa, baada ya kocha Arsene Wenger kumfanya Jovetic mchezaji nambari moja katika orodha ya nyota anaowataka kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao.
  Lakini mpango huo unaelekea kubuma, kutokana na klabu hiyo ya Serie A kugoma kuchukua kiasi chochote cha fedha chini ya Pauni Milioni 25 walizotaka.
  Breaking point: Arsenal's long-term interest in Fiorentina's Stevan Jovetic could have halted over the £25m fee
  Ubakhili utawakosesha kifaa hiki: Mchezaji anayetakiwa kwa muda mrefu Arsenal, Stevan Jovetic wa Fiorentina anauzwa Pauni Milioni 25

  Mabosi wa Gunners, wameiambia Fiorentina wako tayari kulipa tu Pauni Milioni 20 ili kumsajili mshambuliaji huyo wa Montenegro na kuna wasiwasi Juventus nao wanamnyatia Jovetic.
  Kama Arsenal, vigogo hao Italia nao wameanzisha mazungumzo na klabu yake juu ya kumsajili Jovetic — lakini inafahamika itakuwa jambo gumu kwa Fiorentina kuwauzia silaha wapinzani wake.
  On his way: Andrey Arshavin (left), training with Jack Wilshere, could sign for Zenit St Petersburg
  Andondoka: Andrey Arshavin (kushoto), akiwa mazoezini na Jack Wilshere, anaweza kutimkia Zenit St Petersburg

  Pamoja na hayo, Juventus wako tayari kutoa dau ambalo Fiorentina wanataka, ili kuwabadilisha mawazo yao.
  Wakati huo huo, Andrey Arshavin, ambaye amemaliza mkataba wake, anatakiwa na Zenit St Petersburg.
  Mshika Bunduki huyo 'aliyetepeta', ambaye analipwa Pauni 90,000 kwa wiki, pia ana za kwenda kucheza Marekani na Mashariki ya Kati.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: UBAKHILI WA ARSENAL HATARINI KUWAKOSESHA BONGE LA KIFAA CHA SERIE A Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top