• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 24, 2013

  ARSENAL MBIONI KUSAJILI BONGE LA BEKI LA KATI


  IMEWEKWA MEI 24, 2013 SAA 8:12 MCHANA
  KLABU ya Arsenal imeripotiwa kukubaliana na vipengele vya uhamisho wa usajili wa beki wa kati wa Swansea, Ashley Williams katika zoezi ambalo litafungua milango ya kuondoka kwa Thomas Vermaelen Emirates.
  Kocha Arsene Wenger anavutiwa mno na Williams, ambaye anaweza kujiunga na Gunners msimu ujao.
  Arsenal ilijaribu bila mafanikio kumsajili beki huyo wa kimataifa wa Wales Januari mwaka huu na na inataraji kufufua mpango wake huo wiki zijazo, lakini Ijumaa ya leo Mwenyekiti wa Swansea, Huw Jenkins amekanusha kufanya mawasiliano yoyote na klabu hiyo.
  Incoming? Arsene Wenger is interested in bringing Swansea defender Ashley Williams to the Emirates
  Anakuja? Arsene Wenger anavutiwa na beki wa Swansea, Ashley Williams amsajili Emirates

  Beki Mbelgiji, Vermaelen anahofia ndoto zake za kucheza Kombe la Dunia zinaweza kuyeyuka kama atabaki Arsenal msimu ujao.
  Nahodha huyo wa Arsenal amesugua benchi miezi miwili ya mwisho huku Laurent Koscielny na Per Mertesacker wakicheza kama mabeki pacha wa kati.
  Vermaelen ameimarika Arsenal na alitaka kubaki kugombea nafasi msimu ujao.
  Lakini wasiwasi wa beki huyo mwenye umri wa miaka 27 ni iwapo Wenger atasajili beki mpya wa kati anaweza kulazimika kurudi benchi.
  Out of favour: Thomas Vermaelen may have to leave Arsenal in order to find first-team football
  Katika wakati mgumu: Thomas Vermaelen anaweza kuondoka Arsenal ili apate timu atakayokuwa anacheza
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ARSENAL MBIONI KUSAJILI BONGE LA BEKI LA KATI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top