• HABARI MPYA

  Alhamisi, Mei 30, 2013

  VITA MPYA YAIBUKA MAN CITY NA MAN UNITED....ZOTE ZATAKA SAINI YA FABREGAS

  IMEWEKWA MEI 30, 2013 SAA 12:00 JIONI
  KLABU za Manchester United na Manchester City sasa zinamgombea kumrejesha katika Ligi Kuu ya England, kiungo wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas msimu ujao.
  Kocha mpya wa United, David Moyes anataka kutoa Pauni Milioni 25 kumnunua kiu ngo huyo wa Barcelona, ambayo iko tayari kumuuza Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal.
  Lakini Man City nao wameonyesha nia ya kumsajili Mspanyola huyo.
  Aiming high: David Moyes wants to bring Cesc Fabregas back to the Premier League
  Cesc Fabregas anaweza kurejea England
  Setting his sights: Moyes is aiming high with his first transfer as United boss
  Moyes anataka Fabregas atue United

  Arsenal walikubaliana na Barca kwamba wao wawe chaguo la kwanza kumrejesha mchezaji huyo England ikitokea Barca wakataka kumuuza Fabregas, lakini Moyes ambaye anamzimikia kwa muda mrefu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, alijaribu kumsajili kwa mkopo wa muda mrefu Everton katika siku zake za mwanzoni Arsenal. 
  Anaweza akawa mwenye bahati katika jaribio lake la pili la kumtwaa mchezaji huyo kutokana na ukweli kwamba safu ya kiungo wa Man United haiko sawa sawa. Pia anawataka mchezaji mwenzake Fabregas wa Barcelona, Thiago Alcantara na Nahodha wa PSV Eindhoven, Kevin Strootman.
  Kiungo Mholanzi Strootman, mwenye umri wa miaka 23, ni mrefu, mwenye umbo la kuvutia ambaye anaweza kucheza vizuri katika ukabaji na uchezeshaji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: VITA MPYA YAIBUKA MAN CITY NA MAN UNITED....ZOTE ZATAKA SAINI YA FABREGAS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top