• HABARI MPYA

  Jumatano, Mei 29, 2013

  MISS UNI COLLEGE KUPATIKANA KESHOKUTWA BILLICANAS

  Mratibu wa Miss Uni- College, Florence Josephat (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Haabri leo asubuhi katika ukumbi wa Much More, Dar es Salaam kuhusu shindano hilo litakalofanyika Mei 31, kwenye ukumbi wa Billicanas. Kulia ni Francissca Mansilo, Mratibu Msaidizi na nyuma ni baadhi ya washiriki kutoka vyo mbalimbali nchini.  
  Na Princess Asia, IMEWEKWA MEI 29, 2013 SAA 1:20 MCHANA
  MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Bernard Paul ‘Ben Paul’, anatarajiwa kuwasindikiza warembo wa kinyang’anyiro cha Redd’s Miss Uni-college Temeke kitakachofanyika kesho katika ukumbi wa Club Bilicanas, jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mratibu wa shindano hilo, Florence Josephat, alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kwamba kilichobaki ni shoo yenyewe ambayo alitamba itakuwa katika ubora wa hali ya juu.
  Alisema kuwa jumla ya warembo 13 wanatarajia kupanda jukwaani siku hiyo, ikiwa ni baada ya kunolewa vilivyo kwa takribani wiki tatu na kwamba wameiva kuwapagawisha watakaofika kushuhudia uhondo huo.
  “Maandalizi yote yamekamilika hivyo tunawaomba wapenzi wa burudani na urembo kwa ujumla kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwani kipenzi cha warembo, Ben Paul, atatoa burudani ya hali ya juu itakayoambatana na shoo kutoka kwa warembo wetu kutoka vyuo vitano vilivyopo Temeke,” alisema.
  Alivitaja baadhi ya vyuo hivyo kuwa ni Chuo Kikuu cha Uganda, TIA, Chuo cha Bandari, DUCE na Chuo cha Utalii, huku akitamba kuwa kutokana na ubora wa warembo walionao, wana imani mwaka huu Redd’s Miss Tanzania atatoka katika kitongoji chao hicho.
  Florence ambaye alikuwa mshiriki wa fainali za Miss Tanzania 2008, aliwataka wapenzi wa urembo na burudani, hasa wanafunzi wa sekondari na vyuo, kujitokeza kwa wingi siku ya shoo yao ili kujionea warembo bomba, huku wakipata burudani ya aina yake.
  Alitaja kiingilio cha shoo yao kuwa ni Sh 10,000 na kwamba mbali ya kinywaji cha Redd’s ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo, wadhamini wengine ni Shome Decoration & Catering, djfetty.blogspot.com na Lamada Hotel.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MISS UNI COLLEGE KUPATIKANA KESHOKUTWA BILLICANAS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top