• HABARI MPYA

  Jumapili, Mei 26, 2013

  REAL MADRID YAWAPA SPURS PAUNI MILIONI 60 KUMNUNUA GARETH BALE


  IMEWEKWA MEI 26, 2013 SAA 10:55 JIONI
  KLABU ya Real Madrid iko tayari kuijaribu Tottenham kwa dau la Pauni Milioni 60 kwa ajili ya kumnunua Gareth Bale.
  Vigogo hao wa Hispania wamekuwa wakimtaka Bale kwa zaidi ya mwaka na kocha mpya, Carlo Ancelotti ni shabiki mkubwa wa winga huyo.
  Real wamepania kuibuka msimu ujao, baada ya msimu huu kushindwa kushinda taji hata moja na Sunday Telegraph limeripoti kwamba, rais wa klabu hiyo, Florentino Perez amemuahidi Ancelotti Bale atapatikana.
  In demand: Gareth Bale has attracted attention from some of Europe's biggest clubs
  Anatakiwa: Gareth Bale anazivutia klabu kadhaa kubwa Ulaya

  Ancelotti anatarajiwa kuchukua nafasi ya Mreno Jose Mourinho Madrid, ambaye anahamia Chelsea baada ya Mtaliano huyo kuonyesha nia yake kuondoka Paris Saint-Germain.
  Spurs inataka kumbakiza Bale na inajiamini inaweza kufanya hivyo licha ya kukosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
  Bale atakuwa na mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo kabla ya kufunguliwa pazia la usajili, kujadili mustakabali wake.
  Bale ameshinda tuzo za Mwanasoka Bora wa Mwaka za PFA na ya Waandishi wa Habari za Soka na kuwa mchezaji wa kwanza wa Spurs tangu Teddy Sheringham kufunga mabao zaidi ya 20 katika msimu mmoja wa Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: REAL MADRID YAWAPA SPURS PAUNI MILIONI 60 KUMNUNUA GARETH BALE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top