• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 24, 2013

  NIYONZIMA AONGEZA MKATABA MIAKA MIWILI YANGA SC

  Haruna Niyonzima (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya Yanga SC, Jangwani wakati akitangazwa kusaini mkataba mpya leo. kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Abdallah Bin Kleb. PICHA KWA HISANI YA GPL.

  IMEWEKWA MEI 24, 2013 SAA 5:00 ASUBUHIHATIMAYE kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhili Niyonzima amesaini mkataba wa miaka miwili zaidi kuendelea kuichezea Yanga SC na klabu hiyo asubuhi ya leo imetangaza rasmi kuongeza mkataba na mchezaji huyo wa zamani wa APR na Rayon za kwao.
  Kulikuwa kuna mvutano mkubwa kati ya Yanga SC na Haruna juu ya mkataba mpya na kiungo huyo ilikuwa aondoke kesho kurejea kwao, bila kusaini mkataba mpya.
  Hata hivyo, kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba Simba SC imemtengea dau la Sh. Milioni 70 na Azam FC pia inamtaka kwa dau nono zaidi, Yanga imekubali kila alichoomba Haruna katika mkataba mpya na wamemalizana. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: NIYONZIMA AONGEZA MKATABA MIAKA MIWILI YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top