• HABARI MPYA

  Alhamisi, Mei 30, 2013

  LAMPARD AINUSURU ENGLAND KULALA NYUMBANI MBELE YA IRELAND

  IMEWEKWA MEI 29, 2013 SAA 5:55 USIKU
  ENGLAND imetoka sare ya 1-1 na Jamhuri ya Ireland katika mchezo wa kirafiki usiku kwenye Uwanja wa Wembley.Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa William Collum wa Scotland, Ireland ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao ugenini, mfungaji Shane Long dakika ya 13, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Seamus Coleman kutoka wingi ya kulia.
  Frank Lampard aliwasawazishia wenyeji dakika 10 baadaye, yaani dakika ya 23 kuftaia kazi nzuri ya Daniel Sturridge ambaye aliambaa uipande wa kushoto wa box, kabla ya kummiminia krosi mfungaji, aliyemtungua kipa Glenn Whelan.
  Ashley Cole alipewa kofia ya dhahabu baada ya kutimiza mechi 100 za timu ya taifa ya England leo. 
  Katika mchezo huo, kikosi cha England kilikuwa: Hart/Foster dk46, Johnson/Jones dk46, Cahill, Jagielka, Cole/Baines dkl54, Walcott, Lampard, Carrick, Oxlade-Chamberlain/Milner dk87, Rooney na Sturridge/Defoe dk33.
  Ireland: Forde, Coleman, O'Shea, St. Ledger, Kelly, Walters/Sammon dk82, McCarthy, Whelan/Hendrick dk74, McGeady/McClean dk68, Long na Keane/Cox dk66.
  Level terms: Frank Lampard (right) pokes home the equaliser for England
  Mwokozi; Frank Lampard aliifungia England bao la kusawazishaHeads I win: Shane Long nods Republic of Ireland ahead at Wembley against England

  Furaha: Shane Long akishangilia bao lake
  Tonderful: Roy Hodgson presents Ashley Cole with a golden cap to mark 100 appearances for England
  Roy Hodgson akimkabidhi Ashley Cole kofia ya dhahabu kwa kutimiza mechi 100 England
  On the slide: Ireland's Stephen Kelly makes a tackle on England's Theo Walcott
  Stephen Kelly wa Ireland akimdhibiti Theo Walcott wa England
  Off target: Wayne Rooney lobs a shot wide of the goal for England
  Wayne Rooney akipiga shuti lililopaa
  Getting shirty: England captain Ashley Cole sees his shirt pulled by Irleand's Seamus Coleman
  Nahodha wa England, Ashley Cole akivutwa jezi na Seamus Coleman wa Ireland
  Taking a tumble: Ireland's Shane Long and England's Gary Cahill battle for an aerial ball
  Shane Long wa Ireland akipambana na Gary Cahill wa England
  Level terms: Frank Lampard (right) pokes home the equaliser for England
  Frank Lampard (kulia) akiisawazishia England
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: LAMPARD AINUSURU ENGLAND KULALA NYUMBANI MBELE YA IRELAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top