• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 27, 2013

  REAL MADRID YAMPA ZIDANE JUKUMU LA KUHAKIKISHA BALE ANATUA BERNABEU


  IMEWEKWA MEI 27, 2013 SAA 1:00 USIKU
  MMOJA wa wachezaji nyota historia ya Real Madrid, Zinedine Zidane amepewa jukumua la kuhakikisha nyota wa Tottenham, Gareth Bale anatua Bernabeu kwa dau la Pauni Milioni 65.
  Gazeti la Hispania, Marca limeripoti kwamba Galactico huyo wa zamani, Zidane  ni mshauri mkuu katika mpango wa usajili huo na anajaribu kumshawishi Rais wa Real Madrid, Florentino Perez kwamba saini ya Bale ni kitu pekee muhimu.
  Zinedine Zidane of Real Madrid
  Tottenham Hotspur's Welsh midfielder Gareth Bale
  Kipaumbele namba 1: Gwiji wa Real na Ufaransa, Zinedine Zidane (kushoto) na mchezaji anayewaniwa na klabu nyingi Ulaya, Gareth Bale (kulia)
  Seal of approval: Zinedine Zidane has said Gareth Bale is more than good enough to play for Real Madrid
  Mpiga debe: Zinedine Zidane amesema Gareth Bale ni zaidi ya bora kiasi cha kutosha kucheza Real Madrid

  "Kitu ambacho kimenivutia kwa ujumla ni kwamba ana muendelezo wa ubora. siyo wa mechi moja au mbili.Zidane ambaye anamzimikia kwa muda mrefu nyota huyo wa Wales, amesema: "Nimekuwa nikiitazama Tottenham kwa sababu Gareth Bale amekuwa akicheza huko. Mbali na Ronaldo na Messi, ndiye mchezaji ambaye amekuwa akinivutia zaidi duniani. Ni wa uhakika,".
  "Anaendeleza kufunga mabao mazuri na muhimu. Ni mwepsi sana, mwenye kipaji na anayevutia.
  "Ndiyo, wachezaji wenye kipaji kama yeye wanaweza kuja Real Madrid. Ni mzuri kiasi cha kutoha kwa Real Madrid? Ndiyo. Ni zaidi ya mzuri kiasi cha kutosha kucheza  Real Madrid.’
  Zidane alikuwa mchezaji mtu muhimu katika biashara ya usajili Madrid tangu astaafu mwaka 2006. Alichangia mno kutua kwa Raphael Varane Bernabeu na ana matumaini ya kumleta Bale katika njia ile ile.
  Impressive: Bale, in action in Spurs' post-season friendly, has impressed Zidane this season
  Kivutio: Bale akiichezea Spurs. Amemvutia Zidane msimu huu
  Lionel Messi
  Cristiano Ronaldo
  Baada ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, Bale ndiye mchezaji anayemvutia zaidi Zidane
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: REAL MADRID YAMPA ZIDANE JUKUMU LA KUHAKIKISHA BALE ANATUA BERNABEU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top