• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 28, 2013

  SPURS YATOA PAUNI MILIONI 1O KUMSAJILI MKALI WA MABAO HISPANIA ALIYEFULIA BARCA


  IMEWEKWA MEI 28, 2013 SAA 10: 50 ALFAJIRI
  KLABU ya Tottenham imeanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili kwa Pauni Milioni 10, mshambuliaji wa Barcelona David Villa na pia wamefufua nia yao ya kumsajili mchezaji wanayemtaka kwa muda mrefu, Leandro Damiao.
  Andre Villas-Boas aliibua nia ya kumsajili ya Villa mapema mwezi huu na sasa klabu yake nchini Hispania iko tayari kuisikiliza Spurs katika mpango wao wa kumnasa mkali huyo wa mabao kwa ajili ya msimu ujao.
  Klabu hiyo ya Nou Camp iko tayari kumuuza mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye amejikuta katika wakati mgumu kupata namba katika kikosi cha kwanza na anaweza akauzwa kwa Pauni Milioni 12.
  Spurs-bound? Barcelona striker David Villa is a target for Tottenham, who rate him at £10 million
  Atatua Spurs? Mshambuliaji wa Barcelona, David Villa anatakiwa Tottenham kwa Pauni Milioni 10
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: SPURS YATOA PAUNI MILIONI 1O KUMSAJILI MKALI WA MABAO HISPANIA ALIYEFULIA BARCA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top