• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 28, 2013

  FALCAO AFAULU VIPIMO MONACO....NA SASA NI MCHEZAJI MPYA MONACO


  IMEWEKWA MEI 28, 2013 SAA 5:00 USIKU
  MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Radamel Falcao amekuwa nyota baab kubwa kujiunga timu mpya iliyopanda Ligi Kuu Ufaransa, maarufu kama Ligue 1, Monaco inayomwaga fedha kama upupu kusajili, baada ya kufaulu vipimo vya afya katika klabu hiyo. 
  Baada ya kuwanasa wachezaji wawili wa Porto, Joao Moutinho na James Rodriguez kwa Pauni Milioni 60 wote Ijumaa, Monaco inamwaga 'mpunga' tena kumsajili kwa miaka minne au mitano nyota huyo wa Columbian, na kumsajili Ricardo Carvalho kwa mkataba wa mwaka mmoja, ambao unatoa nafasi ya kuongeza mwaka mmoja. 
  Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, Falcao unampa uhuru wa kuondoka katika mwaka wa kwanza wa kuwapo katika klabu hiyo, limesema gazeti la AS la Hispania.
  Monaco bound: Atletico Madrid's Radamel Falcao has passed a medical and looks set to leave Spain
  Monaco wamelamba dume: Radamel Falcao wa Atletico Madrid anahamia Ufaransa.

  Wakala Jorge Mendes wa Falcao na mmiliki wa Monaco, Dmitry Rybolovlev watamalizana juu ya vipengele vingine katika makubalino. 
  Atletico, ambayo Falcao ameichezea kwa misimu miwili akiifungia mabao 70 katika mechi 88, itapata zaidi ya Pauni Milioni 50 katika mauzo ya mchezaji huyo. 
  Kipengele kimoja katika mkataba huo ambacho kimefungwa ni mshahara na Falcao atakuwa anapata jumla ya Pauni Milioni 8.5 kwa msimu baada ya kodi. Carvalho, mwenye umri wa miaka 35, ambaye amemaliza mkataba wake Real Madrid baada ya misimu mitatu atatua kama mchezaji huru Ufaranmsa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: FALCAO AFAULU VIPIMO MONACO....NA SASA NI MCHEZAJI MPYA MONACO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top