• HABARI MPYA

    Friday, April 05, 2013

    TORRES APIGA MBILI CHELSEA IKIUA 3-1, SPURS SARE GARETH BALE AKIUMIA NA PAPPIS CISSE AITENGENEZEA MAZINGIRA NEWCASTLE ULAYA


    MSHAMBULIAJI Fernando Torres jana alikuwa shujaa wa Chelsea akifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Rubin Kazan kwenye Europa League Uwanja wa Stamford Bridge.
    Wiki tatu zilizopita, Torres aliipeleka Chelsea Robo Fainali ya michuano hiyo kwa kufunga bao la ushindi dhidi ya Steaua Bucharest na usiku wa jana mchezaji huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni 50 akiwa amevaa mask usoni aliwatungua mara mbili Rubin Kazan.
    Alifunga bao la kwanza dakika ya 16 akiwa amekaa uwanjani na akapachika la tatu kwa kichwa dakika ya 70, wakati bao la pili la The Blues lilifungwa na Victor Moses dakika ya 32 na bao la kufutia machozi la wapinzani wao lilifungwa na Natcho kwa penalti dakika ya 41.
    Kikosi cha Chelsea jana kilikuwa: Cech, Azpilicueta, Terry, Luiz, Bertrand, Ramires, Lampard, Moses/Hazard dk65, Benayoun/Marin dk83, Mata/Oscar dk78 na Torres. 
    Rubin Kazan: Ryzhikov, Cesar Navas, Kuzmin/Kasaev dk82, Kaleshin, Ansaldi, Sharonov, Orbaiz, Roman Eremenko, Karadeniz, Natcho, Dyadyun/Rondon dk46.

    Masked marauder: Torres is mobbed after scoring his first
    Sura ya ajabu: Torres akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao la kwanzaOpener: Torres slides in to give Chelsea the lead
    Bao la kwanza: Torres akiwa chini akifunga bao la kwanza
                                                                                      Katika mechi nyingine ya michuano hiyo, Tottenham Hotspur ililazimishwa sare ya 2-2 na FC Basle siku ambayo mchezaji wake hatari Gareth Bale aliumia kifundo cha mguu mwishoni mwa mchezo na atakosa mechi ya marudiano.                                                                Mabao ya Spurs yalifungwa na Adebayor dakika ya 40 na Sigurdsson dakika ya 58, wakati ya Basle yalifungwa na Stocker dakika ya 30  na Frei dakika ya 35.
    Just about: Adebayor scored Tottenham's first of the night in the second half
    Adebayor akiifungia Tottenham bao la kwanza

    Newcastle ilifungwa 3-1 na Benfica nchini Ureno, huku bao lake muhimu la ugenini likifungwa na Papiss Cisse’ dakika ya 12, likiwa bao la kwanza kabisa kwenye mchezo huo.
    Mabao ya wenyeji yalifungwa na Rodrigo dakika ya 25, Lima dakika ya 65 na Cardozo dakika ya 71 kwa penalti.
    Katika Robo Fainali nyingine, bao pekee la Dick Kuyt dakika ya 90 liliipa  Fenerbahce ushindi wa 1-0 dhidi ya Lazio.
    Take that! Newcastle's Papiss Cisse, celebrates next to Benfica's Luisao after scoring the opening goal against Benfica
    Chukua hiyo! Mchezaji wa Newcastle, Papiss Cisse, akishangilia baada ya kufungua mbele ya mchezaji wa Benfica, Luisao

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TORRES APIGA MBILI CHELSEA IKIUA 3-1, SPURS SARE GARETH BALE AKIUMIA NA PAPPIS CISSE AITENGENEZEA MAZINGIRA NEWCASTLE ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top