Washambuliaji wawili wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu (kushoto) na Mbwana Samatta (kulia), leo wanatarajhiwa kuiongoza klabu yao, Tout Puissant Mazembe katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mochudi Centre Chiefs ya Botswana mjini Lubumbashi. Mazembe ilishinda 1-0 ugenini, bao pekee la Samatta na leo wakiwa nyumbani, mvua ya mabao inatarajiwa kuwanyeshea Waswana.