![]() |
| Wachezaji wa Taifa Stars wakiwa mazoezini Uwanja wa Karume, Dar es Salaam kanla ya kwenda Msumbiji. Anayekokota mpira ni Mbwana Samatta akijaribu kumtoka beki Juma Nyosso. |
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imewasili mjini Maputo saa 5 asubuhi ya leo kwa saa hapa tayari kwa mechi dhidi ya Msumbiji, The Mambas kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani Afrika Kusini.
Stars iliyoondoka Dar es Salaam leo asubuhi, ilipopokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo na Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi Nyandugu, ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 chini ya Kocha Mkuu, Mdenmark Kim Poulsen na imefikia katika hoteli 2010 LDA iliyoko karibu na Uwanja wa Taifa Zimpeto ambako mechi hiyo itachezwa Jumapili kuanzia saa 9 kamili kwa saa za hapa ambapo Tanzania itakuwa saa 10 kamili.
Kwa mujibu wa programu ya Kocha Kim, timu hiyo itafanya mazoezi leo na kesho katika muda ule ule wa mechi ya Jumapili ambayo itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar. Hadi timu inawasili hapa, hakuna mchezaji yeyote mwenye matatizo ambayo yanaweza kusababisha asicheze mechi ya Jumapili.
Katika mchezo huo, Stars inahitaji ushindi au sare ya mabao yasiyopungua 2-2 ili kupata fursa ya kupangwa katika makundi ya kuwania tiketi ya AFCON mwakani, baada ya mechi ya kwanza kulazimishwa sare ya 1-1 mjijni Dar es Salaam.



.png)
0 comments:
Post a Comment