• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 25, 2012

  VENUS WILLIAMS ANUSA TU KUAGA WIMBLEDON


  Venus Williams akiaga baada ya kutolewa usiku huu

  KATIKA miaka 15 tangu apoteze mechi ya kwanza ya Wimbledon, Venus Williams alitwaa mataji matano ta All England Club na kujitambulisha kama mmoja wa wachezaji wakali wa tenisi kihistoria.
  Tangu hapo, hakuwahi kufungwa tena mechi ya raundi ya kwanza hadi leo.
  Williams ametolewa katika raundi ya ufunguzi ya michuano ya Wimbledon kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1997, akifungwa na Elena Vesnina kwa 6-1, 6-3. Yalikuwa ni matokeo ya kwanza mabaya zaidi kwa Williams kwenye michuano hiyo na pia ilikuwa mara ya nne kufungwa katika raundi ya kwanza katika Grand Slam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VENUS WILLIAMS ANUSA TU KUAGA WIMBLEDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top