• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 28, 2012

  MUDDE ATUA, APEWA JEZI YA YONDAN


  Mudde

  Na Prince Akbar
  KIUNGO wa kimataifa wa Uganda, Mussa Mudde aliyesajiliwa na mabingwa wa soka Tanzania, Simba SC kutoka Sofapaka ya Kenya, amewasili mchana huu kujiunga na wenzake kuendelea na maandalizi ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, imeelezwa.
  Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga ‘Mr Liverpool’, ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba, Mudde amewasili na kukabidhiwa jezi ya Kelvin Yondan aliyehamia Yanga na atakuwapo mazoezini joini hii TCC Chang’ombe, Dar es Salaam.
  Mbali na Mudde, pia mshambuliaji wao waliyemsajili kutoka Dong Tam Long An ya Vietnam, Danny Mrwanda anaanza mazoezi rasmi leo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MUDDE ATUA, APEWA JEZI YA YONDAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top