• HABARI MPYA

    Friday, June 22, 2012

    SIMBA WAPOKEWA KIFALME MWANZA


    Kikosi cha Simba msimu uliopita

    Na Princess Asia
    MABINGWA wa soka Tanzania, Simba SC wamepokea kwa furaha mjini Mwanza walikowasili leo, walkitokea Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya kutembeza Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu na pia kucheza mechi za kirafiki.
    Msemaji wa Simbs SC, Ezekiel Kamwaga ameiambia BIN ZUBEIRY kutoka Mwanza mida hii kwamba timu imefika salama tayri kwa mchezo wao wa kwanza kesho dhidi ya Toto African na Jumapili itacheza na mabingwa wa Uganda, Express kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
    Simba imekwenda Mwanza bila nyota wake wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ambao wamekuwa mapumziko hadi Jumatatu.
    Hao ni Nahodha Juma Kaseja, Haruna Moshi ‘Boban’, Mwinyi Kazimoto na Amir Maftah ambao walirejea nchini juzi kutoka Msumbuji walipokwenda kucheza na wenyeji wao ‘Mambaz’ katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika (AFCON) zitakazopigwa mwakani nchini Afrika Kusini, ambapo ilitolewa kwa mikwaju ya penalti. 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA WAPOKEWA KIFALME MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top