• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 24, 2012

  NDONDI FRIENDS CORNER LEO MASHALI NA SAMSON MAWE


  Mashali kushoto na Samson kulia baada ya kupima uzito jana

  Na Princess Asia
  MABONDIA Thomas Mashali na Maisha Samson wanapanda ulingoni leo katika ukumbi wa ukumbi wa Friends Corner Hotel, Manzese katika pambano la ubingwa wa Taifa, uzito wa Middle, unaotambuliwa na Chama cha Ngumi (TPBO) chini ya rais wake, Yassin Abdallah.
  Mabondia hao jana walipima uzito na wote wakapata kilogramu stahili 71 tayari kwa pambano hilo la raundi 10.
  Mbali na pambano hilo, kutakuwa mapambano ya utangulizi kati ya
  Juma Fundi na Shaaban Madilu, Mohamed Shaaban 'Ndonga' na Mussa Hassan, Jonas Godfrey na Venance Mponji, Abdallah Mohamed 'Prince Naseem' na Yohana Mathayo raundi sita kila pambano, Nassor Hatibu na Abdul Athuman, Martin Richard na  Hassan Kadenge, raundi nne kila pambano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NDONDI FRIENDS CORNER LEO MASHALI NA SAMSON MAWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top