Tetesi za J'mosi magazeti ya Ulaya


CHELSEA YAIPIGA BAO REAL MADRID, YAKARIBIA KUMNASA LUCA MODRIC


KLABU ya Chelsea inakabiria kuipiga bao Real Madrid katika kuinasa saini ya Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26, wakiwa wanaandaa dau la pauni Milioni 36 kumnasa kiungo huyo.
NYOTA Ibrahim Afellay yuko tayari kuzungumzia mustakabali wake katika klabu ya Barcelona - na Tottenham na Liverpool zinafuatilia maendeleo ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 26.
KLABU ya Manchester United imepiga hatua katika harakati zake za kumtaka Leighton Baines na inamtaka mchezaji huyo iondoke naye katika ziara yake ya kujiandaa na msimu mpya Julai 16.
KOCHA wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas anataka mchezaji wa Porto, Joao Moutinho, mwenye umri wa miaka 25, awe wa kwanza kumsajili katika klabu yake mpya, Tottenham kwa dau la pauni Milioni 32 azibe pengo la Luka Modric.
Joao Moutinho
Joao Moutinho 
NYOTA wa Spurs, Giovani Dos Santos, mwenye umri wa miaka 23, anatarajiwa kuondoka White Hart Lane kwenda ama Sevilla au Atletico Madrid mwishoni mwa wiki.
KLABU za Fulham na Everton zinaelezwa kumuwania veki wa Jamhuri ya Czech, Tomas Sivok, mwenye umri wa miaka 28, ambaye yuko huru baada ya mkataba wake wa sasa na klabu yake, Besiktas kufikia tamati.
NYOTA Ezequiel Lavezzi amekataa mpango wa kuhamia Manchester City na kuamua kujiunga na Paris St Germain. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, yuko tayari kukubali uhamisho wa dau la pauni Milioni 21 kwenda klabu hiyo ya Ufaransa.
KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers anamtolea macho, mchezaji wa Bolton, Mark Davies, mwenye umri wa miaka 24, kwa uhamisho wa dau la pauni Milioni 6, baada ya kumkosa Gylfi Sigurdsson.
WAKUU wa klabu ya Newcastle United, wamesafiri hadi Uholanzikujadili mpango wa kumsajili Luuk De Jong, mwenye umri wa miaka 21, kutoka FC Twente ya huko.
KOCHA wa Stoke, Tony Pulis amejiunga kwenye mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Wolves mwenye thamani ya pauni Milioni 10, Steven Fletcher, mwenye umri wa miaka 25 akikimbizana na Sunderland.

EURO 2012

MSHAMBULIAJI wa Italia, Mario Balotelli hana mpango wa kurejea Italia - kwa sababu anafikiri mashabiki wa Manchester City wataendelea kumpenda hata kama waliwang'oa England kwenye Euro 2012.
Mario Balotelli
Mario Balotelli 
MSHAMBULIAJI Sergio Ramos amesema hataki penalti mwishoni mwa fainali ya Euro 2012 na amewaonya Hispania lazima wamzime "wa kipekee" kiungo mkongwe Andrea Pirlo.
KIUNGO wa Hispania, Cesc Fabregas amesema kwamba Mario Balotelli ni tishio kubwa kwa Hispania katika harakati zake za kuweka historia.
KOCHA wa Italia, Cesare Prandelli amesema kwamba wachezaji wake wa Italia hawaihofii Hispania na watatumia muda mwingi kabla ya fainali ya Euro 2012 kuungalia udhaifu wao.
BALE NJE OLIMPIKI
KIUNGO Gareth Bale atakosa michuano ya soka ya Olimpiki baada ya kuumia.
KOCHA Andre Villas-Boas atapoteza kiasi cha pauni Milioni 11, mara atakapotangazwa kuwa kocha mpya wa Tottenham wiki ijayo, kwa sababu alikuwa hajalipwa baadhi ya mafao yake baada ya kufukuzwa Chelsea.
AKIWA bado kocha wa Spurs, Harry Redknapp alijaribu kutaka kumsajili mshambuliaji mtata, Mario Balotelli kwa mkopo kabla ya Mtaliano huyo mwenye asili ya Ghana, mwenye umri wa miaka 21 hajahamia Manchester City mwaka 2010.

COLE, YOUNG WAPEWA PIZZA.

BEKI Ashley Cole na winga Ashley Young wanatakiwa kufanya tangazo la Pizza Hut tangu mwaka 1996, baada ya kukosa penalti zao katika Euro 2012.