• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 26, 2012

  PREVIEW HISPANIA NA URENO KESHO


  Spain vs France - Euro 2012
  Wachezaji wa Hispania

  VIKOSI VYA LEO

  PORTUGAL

  Rui Patricio
  Pereira, Pepe, Alves, Coentrao
  Moutinho, Veloso, Meireles
  Nani, Almeida, Ronaldo

  SPAIN


  Casillas
  Arbeloa, Ramos, Pique, Alba
  Busquets, Alonso
  Silva, Xavi, Iniesta
  Torres


  URENO na Hispania zinafufua upinzani wao, zote zikitoka kushinda mechi tatu mfululizo katika Euro 2012 baada ya mechi za ufunguzi kufungwa na Ujerumani na sare na Italia.
  Kocha wa Seleccao, Paulo Bento bado ni mwenye kujiamini licha ya kuwa hatarini kuwakosa Ricardo Quaresma na Miguel Lopes walioumia mazoezini Jumamosi, lakini atalazimika kufanya mabadiliko baada ya beki wa kati, Helder Postiga kuumia katika mechi dhidi ya Jamhuri ya Czech na nafasi yake itachukuliwa na ama Hugo Almeida au kinda Nelson Oliveira katika kikosi cha kwanza.
  Wakati huo huo, wachezaji wengine kikosini wanatarajiwa kuwa wale wale, huku Cristiano Ronaldo, ambaye hadi sasa amefunga mabao matatu katika mechi mbili zilizopita, Pepe na Fabio Coentrao wakikabiliana na wachezaji wenazao kadhaa wa Real Madrid na wapinazani wa katika Clasico, Barcelona katika kikosi cha Hispania.
  Kizazi cha wachezaji wa Hispania kinatinga Nusu Fainali baada ya kuwatoa Ufaransa na kinatazamiwa kubeba mwali wa michuano hii, baada ya kufanya hivyo katika Euro 2008 na Kombe la Dunia 2010. 
  Lakini, kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari havivutiwi na uchezaji wao, vikisema unaboa, na vinahoji kama timu hiyo ipo kwenye kiwango kile kile kizuri kama ilivyokuwa miaka michache iliyopita.Kocha Vicente del Bosque hawezi kuzifanyia kazi shutuma hizo kwa sasa, na anatarajiwa kuendelea na wachezaji wake wale wale na mfumo ule ule pia, ambao umemfikisha hatua hii. La Roja wamemuanzisha Cesc Fabregas katika mshambuliauji namba moja (Namba.9) katika mechi mbili na baadaye katika mechi mbili wakamuweka Fernando Torres mwenye namba yake na hadi sasa wachezaji wote hao wawili, kila mmoja amefunga mabao mawili. Pamoja na hayo, nyota huyo wa Chelsea ana nafasi kubwa ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza kesho.


  JE WAJUA?

  • Ureno imetumia kikosi kile kile katika mechi zote nne za michuano hiyo hadi sasa.
  • Cristiano Ronaldo (pichani kulia) kwa sasa anafungana kwa mabao katika nafasi ya tatu ya wafungaji wa kihistoria wa michuano hiyo ya Ulaya na washambuliaji sita, nyuma ya Michel Platini na Alan Shearer.
  • Kikosi cha Paulo Bento kimegongesha mwamba mara sita katika michuano hiyo ya Ulaya, hiyo ikiwa ni rekodi mpya, huku mara nne akifanya hivyo Ronaldo.
  • Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana, Ureno ilishinda 4-0 na ilikuwa Novemba mwaka 2010 katika mchezo wa kirafiki, miezi michache baada ya Hispania kuwatoa Ureno katika Kombe la Dunia kwa kuwachapa bao 1-0.
  • Hispania ina rekosi ya jumla ya kucheza mechi 34 na Ureno (imeshinda 16 sare 12 na kufungwa 6). Pamoja na hayo, La Roja imeshinda mechi mbili tu katika mechi 12 zilizopita walizokutana na Seleccao.
  • Mabao mawili ya Xabi Alonso dhidi ya Ufaransa katika Robo Fainali, yalikuja katika siku ambayo alikuwa anaichezea nchi yake mechi ya 100.
  • Hispania imeonyesha ina ukuta bora zaidi katika Euro 2012, kwani hadi sasa, imeruhusu nyavu zake kuguswa mara moja tu na haijafungwa bao ndani ya dakika 299 sasa.
  • Kikosi cha Vicente del Bosque kinaonekana kipo sawa sawa. Mabao matano kati ya mabao yao nane katika Euro 2012 yamekuwa wakipatikana dakika 30 za mwisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PREVIEW HISPANIA NA URENO KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top