• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 29, 2012

  SIMBA KUANZA NA URA, YANGA NA WARUNDI KAGAME, AZAM WAPEWA WAZENJI


  Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye kulia akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za TFF, mchana huu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah.

  Na Prince Akbar
  MABINGWA watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame watafungua dimba na Atletico ya Burundi katika mchezo wa Kundi C wa michuano hiyo, Julai 14, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati wapinzani wao wa jadi, Simba SC waliowekwa Kundi A, wataanza na URA ya Uganda Julai 16, kwenye Uwanja huo huo.
  Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano hiyo, Azam FC wao wataanza na Mafunzo ya Zanzibar katika mchezo wa Kundi B, Uwanja wa Chamazi, Julai 15.
  Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholaus Musonye amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari mchana huu, ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam kwamba, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) itashiriki kama timu mualikwa.
  Aidha, habari za kusikitisha ni kwamba, Musonye amesema Sudan, Ethiopia, Eritrea na Somalia hazitaleta wawakilishi wao kwa sababu mbalimbali.
  Wakati Ethiopia ligi yao inaanza wiki hii, Sudan wawakilishi wao wapo kwenye michuano ya Afrika na wameshindwa kuteua timu mbadala, Somalia wawakilishi wao Elman wamebadilisha uongozi, hivyo bado hawajajipanga na Eritrea kutokana na desturi ya wachezaji wao kuzamia kila wanapokuja kwenye mashindano, wameondolewa.
  “Wameondolewa, kwa sababu mbili, kwanza nchi yao imeomba ipewe muda kulifanyia kazi sual hilo, na sisi pia (CECAFA) tunalitafutia ufumbuzi,”alisema Musonye.  
  Lakini Musonye amekiri kitendo cha kuyatoa mashindano hayo mwanzoni mwa mwaka hadi katikati ya mwaka kumechangia baadhi ya timu kutoshiriki na amesema tayari amewasilisha pendekezo kwenye Mkutano Mkuu, mashindano yarejee kufanyika mwanzoni mwa mwaka kama ilivyokuwa awali.
  Kuhusu mechi ya ufunguzi ya Simba kuchezwa Julai 16, ambayo itakuwa Jumatatu badala ya Jumapili, Musonye alisema kwamba imetokana na kwamba Julai 15, Uwanja wa Taifa kutakuwa na fainali za Copa Coca Cola, ambayo maandalizi yake yote yamekamilika.
  Yanga ndiye bingwa mtetezi wa mashindano, baada ya kuifunga Simba SC katika fainali mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  CECAFA CLUB KAGAME CUP 2012
  14th – 28th July 2012, Dar-Es Salaam, Tanzania
  Team Fixture list
   
  GROUP A             SIMBA(TZ), URA (UGA), VITA CLUB (CONGO DR) PORTS (DJB),
  GROUP B             AZAM(TZ), MAFUNZO(ZANZ), TUSKER (KEN),  
  GROUP C             YANGA(TZ), APR(RWD),WAU SALAAM (SOUTH SUDAN), ATLETICO(BUR),
   
  (QUALIFICATION: GROUP A 1st and 2nd AND 3rd GROUP B 1st and 2nd , GROUP C 1st and 2nd  AND 3rd QUALIFY TO QUARTER FINALS).
   
  DATE
  NO
  TEAMS
  GROUP
  VENUE
  TIME (EAT)
  Sat 14th July
  1
  2
  APR Vs WAU SALAAM
  YANGA v ATLETICO
  C
  C
  Dar
  Dar
  2pm
  4 PM
  Sun 15THJuly
  3
   
  AZAM V MAFUNZO
   
  B
   
  CHIMANZI
  4 PM
  Mon 16th July
  4
  5
  VITA CLUB Vs PORTS
  SIMBA Vs URA
  A
  A
  Dar
  Dar
  2PM
  4PM
  Tue 17th July
  6
  7
  ATLETICO Vs APR
  WAU SALAAM Vs YANGA
  C
  C
  Dar
  Dar
  2pm
  4PM
  Wed 18th July
  8
  9
  VITA CLUB Vs URA
  PORTS  Vs SIMBA
  A
  A
  Dar
  Dar
  2 pm
  4pm
  Thu 19th July
  10
  11
  ATLETICO Vs WAU Salam
  MAFUNZO Vs TUSKER
  C
  B
  Dar
  Dar
  2pm
  4pm
  Fri 20th July
  12
  13
  PORTS Vs URA
  YANGA Vs APR
  A
  C
  Dar
  Dar
  2pm
  4pm
  Sat 21st July
   
  14
  15
   
   
  AZAM Vs TUSKER
  SIMBA Vs VITA CLUB
   
   
  B
  A
   
   
  TBD
  TBD
  TBD
  TBD
   
  TBD
  Sun 22nd July
   
  REST DAY
   
   
   
   
   
  QUARTER FINALS
  Mon 23th July
  16
  17
  B2 Vs C2
  A1 Vs C3
   
   
  TBD
  TBD
  Tue 24th July
  18
  19
  C1 Vs A2
  B1 VsA3
   
  TBD
  TBD
  Wed 25th July
   
  REST DAY
   
   
  SEMI FINALS
  Thu 26th July
  20
  Winner 16 Vs Winner 17
   
  TBD
  TBD
  Thu 26th July
  21
  Winner 18 Vs Winner 19
   
  TBD
  TBD
   Fri 27th July
  REST DAY
  FINALS AND 3rd PLACE PLAY OFFS
  Sat 28th July
  22
  23
  Loser 20 Vs Loser 21
  Winner 20 Vs Winner 21
   
   
  TBD
  TBD
   

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA KUANZA NA URA, YANGA NA WARUNDI KAGAME, AZAM WAPEWA WAZENJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top