• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 27, 2012

  MASHUJAA BAND WAVAMIA KAMBI YA SIMBA


  Martine Sospeter

  Na Princess Asia
  BENDI ya muziki wa dansi Mashujaa Wanakibega' Jumapili hii itaanza bonanza maalum katika viwanja vya TCC Club Chang'ombe Dar es Salaam, ambako mabingwa wa soka Tanzania, Simba SC wameweka kambi yao ya mazoezi kwa sasa.
  Akizungumza Dar es Salaam jana meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter, alisema kuwa kwa kuanzia Jumapili hii ya Julai mosi itakuwa ikifanya maonesho yake uwanjani hapo.
  Sopeter alisema kuwa bendi hiyo itakuwa na bonanza lake maalum ambalo linajulikana kama (Mashujaa Sunday Soccer Bonanza) itakayokuwa ikifanyika hapo kila Jumapili.
  Alisema burudani kutoka kwa bendi hiyo itaanza saa 9.Alasiri na kumalizika saa 3,usiku.
  "Tumejipanga kuwapa wakati wa temeke burudani ndiyo maana tumeamua kuleta burudani hiyo kila Jumapili na itakuwa ikifanya maonyesho yake kwa zaidi ya masaa saba ili kila mmoja aweze kuridhika na onesho letu"alisema Sospeter.
  Alisema bendi hiyo chini ya Rais Chalz Baba imejipanga kuhakikisha inatoa burudani mwanzo mwisho na kuridhisha wapenzi wao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASHUJAA BAND WAVAMIA KAMBI YA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top