• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 29, 2012

  WEMA AMZAWADIA OMOTOLA SHANGA


  Mwigizaji Omotola Jalade wa pili kushoto akikabidhiwa zawadi na za khanga, shanga na viatu Wema Sepetu wakati akiondoka kuelekea Nigeria jana usiku. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole ambao waliratibu ziara ya msanii huyo. Mwingine wa msanii Snura.

  Omotola akijaribu bangili za kimasai alizopewa kama zawadi
  Mwigizaji Wema Sepetu akimvalisha Khanga Omotola Jalade muda mfupi kabla ya hajandoka nchini kuelekea Nigeria.
   
  Na Princess Asia
  MWIGIZAJI  maarufu kutoka Nigeria Omotola Jalade Ekeinde aliondoka nchini jana usiku na kuahidi kusaidia soko la filamu nchini liweze kufikia ngazi za kimataifa.
  Akizungumza na Mkurugenzi wa kampuni ya One Touch Solutions, Petter Mwendapole iliyoratibu ziara yake pamoja na mwigizaji Wema Sepetu aliyekuwa mwenyeji wake, Omotola alisema Tanzania ina kila sababu ya kuwika kimataifa katika filamu.
  “Kwa Afrika Tanzania inaweza kuwa namba moja kama Nigeria, mna hali ya hewa nzuri, vivutio vya utalii na pia mna waigizaji ambao wana vipaji, hii inaweza kuwapeleka mbali yapo mambo madogo ya kurekebisha,” amesema.
  Alisema kwa kuanzia atafanya kazi kwa karibu na Wema Sepetu ambaye ndiye alikuwa mwenyeji wake na kuhakikisha anafikia mafanikio ya juu katika tasnia hiyo kwa kimataifa.
  Omotola mama wa watoto watatu, alisema kwa Nigeria yeye anafahamika kama Super Star hiyo alipoambiwa anakuja kuzindua filamu ya jina hilo alijiona kuwa ni muhisika wa moja kwa moja.
  Tangu kuwasili kwake nchini vyombo mbalimbali vya habari vya Nigeria vimekuwa vikatangaza na kuzipa taarifa za uzinduzi wa filamu ya super star nafasi kubwa.
  Akiwa nchini alitembelea kituo cha watoto yatima kinachohudumiwa na Tanzania Mitindo House, kabla ya kula chakula cha mchana na watoto hao nyumbani kwa Wema na jioni yake kuzindua filamu katika hoteli ya Giraffe. Pia alitembelea jengo la Quality Plaza ambapo alikwenda kuangalia sinema.
  Wakati akiondoka, Omotola alikabidhiwa Khanga, viatu vya kimasai na shanga. Mbali na Wafanyakazi wa One Touch na Endless Fame na Image Professional mwigizaji mwingine maarufu nchini na Mkurugenzi wa 5 Effect, Gabriel Mtitu alikuwepo uwanjani hapo kumsindikiza na walizungumza mambo kadhaa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WEMA AMZAWADIA OMOTOLA SHANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top