• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 26, 2012

  TWANGA PEPETA NDANI YA MISS KANDA YA KATI, WABUNGEEEE


  Mwimbaji nyota wa Twanga Pepeta, Janet Isinike 'Janet Jackson'

  Na Princess Asia
  BENDI ya African Stars Band ‘Twanga Pepeta’ Ijumaa ya wiki hii tarehe 29-06-2012 itatoa burudani katika kinyang'anyiro cha kumsaka Redds Miss Kanda ya Kati onyesho litakalofanyika Mkoani Dodoma.
  Onyesho hilo linataraji kufanyika siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Club Kilimani. Shindano la Miss Kanda ya Kati ni majumuisho ya washindi watatu walioshinda kutoka katika Mikoa ya Redds Miss Tabora, Redds Miss Singida, Redds Miss Dodoma na Redds Miss Kigoma yaliyofanyika hapo awali, Washindi watatu wa Redds Miss Kanda ya Kati wataungana na wenzao kutoka katika kanda nyingine ili kushiriki Shindano la Redds Miss Tanzania litakalofanyika hapo baadae mwaka huu.
  Twanga inataraji kutumia fursa hiyo ili kuitambulisha single yao iliyokamata Jiji kwa sasa ya 'Shamba la Twanga' kwa wapenzi wake wa Dodoma pia tunataraji kuwaalika Waheshimiwa Wabunge wanaohudhuria vikao vya Bunge la Budget ili nao wapate fursa  kusikia single ya Shamba la Twanga.
  Mgeni rasmi katika onesho hilo anataraji kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk. Fenella Mukangara.
  Twanga Pepeta wanataraji kuondoka siku ya Ijumaa alfajiri mara baada ya kumalizika kwa onyesho Club Maisha na watarejea jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi kuendelea kutoa burudani katika ukumbi wao nyumbani wa Mango Garden au maarufu kama 'Twanga City'.
  Twanga itapeleka kikosi chake chote kilichosheheni wanamuziki wake nyota watakaoongozwa na Meneja wa Bendi Khamis Amigo na Kiongozi luizer Mbutu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TWANGA PEPETA NDANI YA MISS KANDA YA KATI, WABUNGEEEE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top