• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 26, 2012

  MARADONA AIWANGIA ITALIA, ASEMA UJERUMANI YA SASA INATISHA


  Diego Maradona - Al Wasl
  Maradona
  GWIJI wa soka Argentina, Diego Maradona ametabiri kwamba Ujerumani inaweza kuifunga Italia katika Nusu Fainali ya Euro 2012 keshokutwa.
  The Azzurri wamekuwa na matokeo mazuri dhidi ya Ujerumani siku za karibuni, kumbukumbu zaidi walipowafunga katika Kombe la Dunia mwaka 2006 mjini Dortmund.
  Licha ya hivyo, Maradona anaamini kwamba kizazi kipya cha Die Mannschaft cha viungo makinda wafungaji kitawapa fursa kuwafunga wapinzani wao na pia anawapa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa. 
  "Nyota wachanga wa Ujerumani [Mesut] Ozil, [Sami] Khedira na [Thomas] Muller wanatisha sana katika zama hizi," ameandika katika gazeti la The Times la India. 
  "Viungo waoa makinda na kufunga kwao kwa urahisi vinawafanya wawe na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa michuano hii, pamoja na kwamba lazima wakutane na mechi ngumu ya Nusu Fainali dhidi ya Italia.
  ITALIA INAAGA?
  8/1Ujerumani inapewa 8/1 kuifunga Italia katika muda wa nyongeza na Sportingbet
  "Kama ni fursa nzuri zaidi daima ya kubadilisha bahati yao dhidi ya The Azzurri, basi ni hii.
  "[Lakini] Ujerumani itafanya vizuri, si kwa kuwadharau wao."
  Pamoja na hayo amempongeza kocha wa Italia, Cesare Prandelli kwa kuifikisha Azzurri Nusu Fainali.
  "Watu wachache sana walitarajia chochote kutoka kwa Italia katika michuano hii ya Ulaya," alisema. 
  "Na [kisha waliokuwa] mabingwa watetezi wa dunia waliboronga katika fainali za Kombe la Dunia zilizopita Afrika Kusini. Kocha Prandelli ameiwezesha timu ya taifa ya Italia iliyokuwa inapondwa na mashabiki Milioni 60 kufanya vizuri"alisema Maradona."
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MARADONA AIWANGIA ITALIA, ASEMA UJERUMANI YA SASA INATISHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top