• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 28, 2012

  RONALDO: MIMI ILIKUWA NIPIGE PENALTI YA TANO


  Euro 2012 : Cristiano Ronaldo (Portugal vs Spain)
  Ronaldo
  Na James Goldman,
   In Donetsk 
  NAHODHA wa Ureno, Cristiano Ronaldo amethibitisha kwamba alikubali kupiga penalti ya tano katika matuta kwenye Nusu Fainali ya kwanza ya Euro 2012 waliyotolewa na Hispania usiku wa kuamkia leo .
  The Seleccao walipoteza mechi hiyo, baada ya Joao Moutinho na Bruno Alves wote kukosa penalti zao, huku Ronaldo - akikosa nafasi ya kupiga penalti ya mwisho kumtungua kipa wa klabu yake, Real Madrid, Iker Casillas.
  "Nilikuwa nakwenda kupiga penalti ya tano, lakini tulikosa mbili," Ronaldo aliwaambia Waandishi. "Lilikuwa ni swali nililozungumza na kocha. Aliniambia: 'Unataka kupiga penalti ya tano?' NIkamuambia ndio.
  "Wakati mwingine napiga ya kwanza, ya pili au ya tatu. Nilikubali kupiga ya tano.
  "Natumai Hispania watachukua ubingwa sasa, kwa sababu nina marafiki wengi kule na itakuwa fainali kali kwao. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO: MIMI ILIKUWA NIPIGE PENALTI YA TANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top