• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 29, 2012

  RIDE & DRIVE YA CFAO MOTORS YAFANA
  1.          Huu ndio msafara wa magari tofauti ya kampuni ya CFAO Motors Group yakiendeshwa na wateja kutoka kampuni tofauti wakati wa Ride & Drive yakiwemo Nissan, Benz, VW ‘AMAROK’ na Suzuki yakichanja mbuga kwenye mabonde na milima kujaribu ubora wake.

  2.          Wateja wa Kampuni ya CFA0 Motors wakibadilishana mawazo kuhusiana na ubora wa magari hayo.

  3.          It’s Ride & Drive time……Kinamama nao wamo.

  4.          Mkurugenzi mpya wa kampuni mpya ya Alliance Motors Bw. Alfred Minja akipozi na gari yake aina Volks Wagon ‘AMAROK’.

  5.          Meneja Masoko mpya wa CFAO Motors, Tharaia Ahmed akizungumzia tukio la Ride & Drive kwa wateja wa CFAO Motors kutoka kampuni  mbalimbali ambapo amewahakikisha ubora wa magari yanayoagizwa na kampuni hiyo na jinsi walivyojidhatiti katika kutoa huduma bora kwa wateja wao.

  6.          Meneja Bidhaa wa CFAO Motors Tanzania Alex Oelofse (mwenye T-shirt nyekundu) akijumuika kupooza makoo na wageni waalikwa baada ya zoezi la Ride & Drive kwa wateja wa kampuni hiyo.

  7.          Mwakilishi wa Masoko wa CFAO Motors Magdalena Mpeku (wa pili kulia) na Tender Manager Bw. Marco Kahabi waki entertain wageni waalikwa baada ya zoezi la Ride & Drive.

  8.          Mkurugenzi Mkuu wa CFAO Motors Uganda  Bw. Eric Ruiz akibadilishana mawazo na Meneja Masoko Mpya wa CFAO Motors Tharaia Ahmed.

  9.          Meneja Masoko mpya wa CFAO Motors Tharaia Ahmed akiteta na mmoja wa wageni waalikwa.
  Na Princess Asia
  KAMPUNI maarufu ya kuuza na kusambaza magari nchini Tanzania ya CFAO Motors kwa mara nyingine imewapa fursa wateja wake kuyajaribu kwa kuyaendesha magari wanayoyauza na gari mpya aina ya Volks Wagon katika viwanja vya maeneo ya Coco Beach.
  Wateja hao kutoka kampuni mbalimbali wamepata nafasi ya kupakia na pia kuyaendesha magari mapya yanayoingizwa hapa nchini na kampuni hiyo ili kujua upya na uimara wa magari hayo hivyo kuweza kuchagua magari bora ya kununua.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY, Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed amesema kampuni hiyo imechagua viwanja hivyo kwa kuwa vina sehemu zenye mawe, miinuko na barabara korofi ili wateja wao waweze kuthibitisha uimara wa magari yanayouzwa na kampuni hiyo.
  Naye Mkurugenzi mpya wa kampuni mpya ya Alliance Motors Bw. Alfred Minja amesema kampuni yake ambayo ni moja ya makampuni ya CFAO Motors Group imeingiza magari mapya aina ya Volks Wagon yakiwemo ‘Amarok’ ikiwa ni katika kuwapatia watanzania nafasi ya kuchagua gari bora wanalolipenda kwa gharama nafuu.
  Nao baadhi ya wateja waliopata nafasi yak u-‘Ride and Drive’ wamesifia ubora na upya wa magari hayo na kuhimiza watanzania na kampuni mbali mbli kununua gari hizo.
  Dereva wa siku nyingi na mwanajeshi wa zamani Bw. Issa Swalehe amesema kuanzia gari kubwa aina ya ‘Benzi Zitros’ ni nzuri hasa katika sehemu sizizopitika kirahisi na gia zake zinaingia kirahisi kama unavyoendesha gari ndogo.
  Kampuni ya CFAO Motors ambayo kwa sasa imefungua kampuni ya Alliance Motors itakayokuwa chini ya Bw. Alfred Minja na kuuza aina tofauti za magari ya ‘Volkswagon’, Nissan, Benzi na mengineyo hufanya tukio kama hilo la kutoa fursa wa wateja wake ku-‘feel’ ubora wa magari hayo mara tatu kwa mwaka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RIDE & DRIVE YA CFAO MOTORS YAFANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top