• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 28, 2012

  JUMA FUNDI ULINGONI JULAI 15 DDC KARIAKOO


  Juma Fundi kushoto akimchapa mtu, je Julai 15 ataendeleza ubabe?

  Na Princess Asia
  BONDIA Juma Fundi anatarajiwa kupanda ulingoni Julai 15, mwaka huu kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo, Dar es Salaam kuzipiga na Baina Mazola katika pambano la uzito wa Bantam, ambalo litasimamiwa na bodi ya ngumi ya TPBO.
  Pambano hilo, limeandaliwa na kampuni ya Kaike Promotions ya Dar es Salaam chini ya Mkurugenzi wake, Siraj Kaike na litatanguliwa na mapambano kadhaa, kati ya Issa Omar wa Big-Right Boxing ya Mwananyamala na Ramadhani Kumbilo wa Keko, Anthony Mathias na Mwaite Juma wa Big Right Boxing.
  Mapambano mengine ni kati ya Doi Miyeyusho na Shaaban Mtengela na Bakari Mohamed na Sadiki Momba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JUMA FUNDI ULINGONI JULAI 15 DDC KARIAKOO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top