• HABARI MPYA

    Friday, June 22, 2012

    WAJANJA WA TOWN LEO WOTE MISS DAR INTER COLLEGE


    Washiriki Miss Dar Inter College, nani ataibuka mshindi leo? Twendeni tukashuhudie

    Na Princess Asia
    Dina 'Dodo'
    HAYAWI hayawi, hatimaye yamekuwa- shindano la Miss Dar Inter College 2012 linatarajiwa kufanyika leo kwenye ukumbi wa Makumbusho, katikati ya Jiji karibu kabisa na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), likisindikizwa na burudani ya Mfalme wa
    Bongo Fleva, Nassib Abdul au Diamond Platinum.
    Diamond ambaye imeelezwa leo atatinga na mkoko wake mpya wa ‘bei chafu’ alioununua hivi karibuni katika shoo hiyo, ili mashabiki wake waune kwa macho yao makavu, amepania kufanya mambo baab kubwa leo Miss Dar Inter College 2012.
    Shindano hilo, litakaloshirikisha mabinti wenye upeo wa hali ya juu kutokana na ukweli kwamba wanatoka vyuoni, mbali na burudani ya Mfalme wa Bongo Fleva, Diamond Platinum, pia litapambwa na burudani ya bendi mpya ya muziki wa dansi inayokuja juu hivi sasa, Skylight.
    Diamond atatinga na mkoko huu leo; umewahi kuuona live?
    Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail Mkingiye ‘Dodo’, ameiambia BIN ZUBEIRY maandalizi kwa ujumla yanaendelea vizuri na warembo 14 watakaoshiriki shindano hilo leo watafanyiwa usaili Dar es Salaam
    “Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Inter College anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania,” alisema.
    Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu Huria (OUT) wakati taji la Miss Inter College linashikiliwa na binti kutoka IFM, Rose Msuya.
    Warembo wawili wa Inter College walishiriki fainali za Miss Tanzania mwaka jana na kufanya vizuri, mbali na Rose mwingine ni mshindi wake wa pili, Blessing Ngowi.
    Dina aliyewahi kuandikia pia magazeti ya Majira, Spoti Starehe na kutangazia Radio Times, aliwataja warembo wanaoshiriki shindano hilo kuwa ni Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacqueline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
    Amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni Redd’s Premium, Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel, Grand Villa Hotel, Clouds Media Group blog za Michuzi, Dina Ismail, BIN ZUBEIRY, Mtaa kwa Mtaa na Full Shangwe.
    Moja ya vitu watavayoonyesha jukwaani leo ni shoo hii; kwa nini ukose?

     CATHERINE CHRISTIAN (OUT)
     DIANA NYAKISINDA (DSJ)
     HILDA EDWARD (USTAWI)
     JACLINE CLIFF (DSJ)
     JAMILA HASSAN (DSJ)
     NANCY MAGANGA
     NATASHA DEO (USTAWI)
     NEEMA MICHAEL (CBE)
     ROSE MASANJA (USTAWI)
     ROSE MUSHUMBUSHI (CBE)
     SAADA SELEMAN (USTAWI )
     SHARIFA IBRAHIM (DSJ)
     NEEMA NGOTA (CBE)
     VERONICA YOLLA (DSJ)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAJANJA WA TOWN LEO WOTE MISS DAR INTER COLLEGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top