• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 26, 2012

  ENHEEE! DIAMOND KAENDA KUSEMA NINI TENA GLOBAL?

  Diamond Platinum akiwa nje za ofisi ya magazeti pendwa, Global Publisher Limited, eneo la Sinza Africasana jioni ya leo. Nilikuwa natoka studio kwa P Funk nikakutana naye nje, baada ya kusalimiana nikamlamba picha. Ni kama kijana alikuwa anawahi interview...sijui amechonga nini, fuatilia magazeti pendwa ujue kafunguka nini. Sijui kuhusu Wema, sijui kuhusu ishu zake. Sijui. Kuanzia kesho, ukiona mzigo kutoka nyumba ya magazeti pendwa, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi we kamata fungua kurasa labda utakutana na interview la Nassib Abdul.  Huyu Mzee, anaitwa Stambuli Mponda, mwanachama maarufu wa Simba SC, alishuka kwenye gari kabla haijasimama ili kuomba kupiga picha na The Platinum. baab kubwa!

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ENHEEE! DIAMOND KAENDA KUSEMA NINI TENA GLOBAL? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top