• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 30, 2012

  YANGA YAICHAPA 2-1 EXPRESS  Mechi kati ya Yanga na Express ya Uganda, imemalizika wenyeji wameshinda 2-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mabao yote yakitiwa kimiani na Jerry Tegete dakika ya nne na 20, wakati la mabingwa wa Uganda, beki Ladislaus Mbogo alijifunga katika harakati za kuokoa mpira wa Kiiza Ayoub dakika ya 77. Kipindi cha kwanza Yanga ilitawala mchezo kwa asilimia 60, Express walipiga krosi mbili na shuti moja ambalo halikulenga lango, lakini kipindi cha pili Express walitawala na dakika 20 za mwisho Yanga walikuwa wanaomba mpira usihe. 
  Kikosi kilichoanza Yanga, kutoka kulia waliosimama Ally Mustafa 'Barthez', Athumani Iddi 'Chuji', Said Bahanuzi, Oscar Joshua, Jerry Tegete na Nizar Khalfan. Walioinama kutoka kulia ni Kelvin Yondan, Nadir Cannavaro, Juma Abdul, Frank Damayo na Simon Msuva. 

  Benchi

  Nizar akimpongeza Tegete baada ya kufunga la pili

  Vijana wanaingia uwanjani

  Wenye timu yao

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA YAICHAPA 2-1 EXPRESS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top