• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 26, 2012

  MAFARAO, NYIGU WADOGO KUCHEZA NA NGORONGORO


  Thomas Ulimwengu, mshambuliaji wa Ngorongoro
  Na Prince Akbar
  TIMU ya soka ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 ya Tanzania, Ngorongoro Heroes itacheza mechi nne za kirafiki na timu za Misri na Rwanda kabla ya kuivaa Nigeria kwenye mashindano ya Afrika.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba Ngorongoro Heroes ambayo kwa mara ya kwanza itakuwa chini ya kocha mpya Jakob Michelsen itaanza kwa kucheza mechi mbili za Misri zitakazofanyika Julai 3 na 5 mwaka huu, na baadaye Julai 14 na 16 mwaka huu dhidi ya Rwanda.
  Amesema mechi zote zitachezwa nchini, na kama ilivyo Ngorongoro Heroes, Misri na Rwanda nazo ziko kwenye kinyang’anyiro cha kusaka tiketi za kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 zitakazofanyika mwakani nchini Algeria.
  Katika raundi ya kwanza, Ngorongoro Heroes iliitoa Sudan ambapo katika raundi ya pili imepangiwa Nigeria, na mechi ya kwanza itafanyika jijini Dar es Salaam, Julai 29 mwaka huu. Timu hizo zitarudiana wiki mbili baadaye nchini Nigeria.
  Iwapo Ngorongoro Heroes itafanikiwa kuitoa Nigeria, katika raundi ya mwisho itacheza na mshindi kati ya Congo Brazzaville na Afrika Kusini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAFARAO, NYIGU WADOGO KUCHEZA NA NGORONGORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top