• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 27, 2012

  DOM YAENDELEA KUTISHA COPA COCA COLA


  Na Princess Asia
  DODOMA imeendeleza wimbi la ushindi kwenye michuano ya Copa Coca-Cola 2012 baada ya leo asubuhi (Juni 27 mwaka huu) kuifunga Mbeya mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tamco ulioko Kibaha mkoani Pwani.
  Mabao ya Dodoma katika mechi hiyo ya kundi C yalifungwa na Japhet Lunyungu dakika ya 59 wakati Frank Kaji aliwahakikishia ushindi washindi dakika saba kabla ya filimbi ya mwisho baada ya kupachika bao la pili.
  Nayo Mjini Magharibi iliifunga Iringa mabao 3-0 katika mechi ya kundi B iliyochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Nyumbu mkoani Pwani.
  Mechi za asubuhi zilizokuwa zichezwe leo kati ya Arusha na Kusini Pemba kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers na Pwani na Tabora kwenye Uwanja wa Karume sasa zitachezwa kuanzia saa 8 mchana kutokana na kutokuwepo mawasiliano ya barabara asubuhi (Morogoro Road) kutoka mkoani Pwani kuingia Dar es Salaam.
  Leo jioni kutakuwa na mechi kati ya Rukwa na Ruvuma (Tanganyika Packers), Mwanza na Tanga (Nyumbu), Kaskazini Unguja na Mara (Tamco) na Singida na Kagera (Karume).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DOM YAENDELEA KUTISHA COPA COCA COLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top