• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 29, 2012

  RAY ATOA FILAMU YA KWANZA TANGU KIFO CHA KANUMBA


  Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabizi sehemu ya msaada uliotolewa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam leo kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre   kilichopo Kinondoni Zainabu Bakari vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye samani ya shilingi milioni moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage.Picha na Mpiga picha Wetu    
  Na Princess Asia
  MSANII wa filamu nchini Vincent Kigosi 'Ray'  amezindua filamu yake  mpya inayojulikana kama 'SOBING SOUND'.
  Filamu hiyo ameizindua kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua ukumbini kama ilivyozoeleka na wengi, msanii huyo amezindua filamu hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni 1.5 kwa niaba ya Kempuni ya Steps Entertainment ya Dar es salaam
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY mara baada ya kuzindua filamu hiyo, akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Ray alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha hHuku wengine wakiendelea kutaabika kitendo ambacho si kizuri.
  Alisema ujio wa filamu hiyo ni kama azma yake aliyoipanga tangu awali kuhakikisha filamu zake zote zinafanya vizuri na atakuwa kila filamu anayotoa atahakikisha japo kidogo kwa namna yoyote anawakumbuka watoto yatima, kwani anawapenda.
  Hii ni filamu ya kwanza Ray anatoa, tangu kifo cha mwigizaji mwenzake wa kiume maarufu, Steven Kanumba aliyefariki dunia, Aprili mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RAY ATOA FILAMU YA KWANZA TANGU KIFO CHA KANUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top