• HABARI MPYA

    Saturday, June 30, 2012

    KASEJA, DAMAYO, AZAM WANG'ARA TUZO ZA LIGI KUU 2012


    Mgeni rasmi, Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye kushoto akiwa na Meneja Masoko wa Vodacom Kevin Twisa 'Kifaa'


    Katikati ni Sumaye, kulia Twisa na kuhsoto Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) na mmiliki wa kituo cha Redio cha Voice Of Tabora

    Ofisa Habari wa TFF, Boniphace Wambura kulia

    Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala kushoto na rafiki zake

    Twisa akihutubia

    Mwenyekiki wa Simba, Rage kulia, Mwenyekiti wa Azam, Mzee Mohamed Said katikati na Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa  

    Waziri Mkuu wa zamani, kipenzi cha Watanzania, Sumaye

    Msaidizi wa Sumaye, Chombo kulia akizungumza na bosi wake

    Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah kulia, katikati Twisa wakiwa na Sumaye

    Wadau, Dina Ismail kushoto na Mohamed Mharizo

    Warembo wa Vodacom

    Maswahiba wa miaka nenda, rudi, Grace Hoka, Mhariri wa BINGWA na Dina Ismail, wa dinaismail.blogspot.com ambaye pia ni Mwandashi wa Habari za Michezo Mwandamizi wa gazeti la Tanzania Daima

    Twisa kulia na Sumaye 

    Rage na Sumaye wakiteta

    Sumaye

    Sumaye

    Sumaye

    Sumaye

    BIN ZUBEIRY

    Mzee Said kulia, Mwesigwa na Jaffar Iddi, Msemaji wa Azam 

    Vimwana wa Vodacom na mataji, tuzo mbalimbali walizokabidhiwa washindi

    Refa bora, Martine Sanya kulia akipokea tuzo yake kutoka kwa Mh Sumaye. Kushoto ni Twisa 

    Rage amkimpokelea tuzo Kaseja

    Mzee Said akipokea tuzo

    Mwesigwa akipokea hundi ya Yanga

    Mzee Said akipokea tuzo ya Azam FC

    Rage akipokea hundi ya Simba SC

    Angetile akipongezana na Mh Sumaye

    Wadau wa Yanga, katika picha ya pamoja na Mh Sumaye

    Wadau wa Simba SC katika picha ya pamoja na Mh Sumaye

    Angetile kulia na kushoto Wambura katika picha ya pamoja na Sumaye
    Frank damayo

    Mlimbwende

    Damayo akipokea tuzo yake

    Damayo akichukua msosi

    Mh Mbunge na kiungo wa zamani wa Simba SC, Rage 'akifakamia' 
    Na Prince Akbar
    JUMA Kaseja, kipa wa Simba SC usiku huu ameibuka kipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kujinyakulia kitita cha Sh. Milioni 3.3 kutoka kwa wadhamini Vodacom.
    Katika hafla ya kukabidhi tuzo za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom zilizofanyika kwenye hoteli ya Double Tree By Hilton, Masaki, Dar es Salaam, beki wa Azam FC, Aggrey Morris alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu wa Ligi Kuu.
    Aidha, Azam FC washindi wa pili wa Ligi Kuu walitwaa pia tuzo za timu yenye nidhamu, wakati kocha waom, Stewart Hall kutoka Uingereza, aliibuka kocha bora, mshambuliaji wake John Bocco ‘Adebayor’ aliibuka mfungaji bora.
    Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah pia alitambulisha tuzo maalum kwa wachezaji chipukizi waliopandishwa kutoka timu za vijana na kufanya vizuri katika timu za wakubwa.
    Katika tuzo hizo, kiungo mpya wa Yanga, Frank Damayo sambamba na Rashid Mandawa wa Coastal Union na Hassan Dilunga wa Ruvu Shooting, kila mmoja alitwaa Sh. Milioni 1.
    Katika hafla hiyo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, mwamuzi Martin Sanya alishinda tuzo ya refa bora, wakati bingwa Simba alizawadiwa Milioni 50, mshindi wa pili Azam Milioni 22 na Yanga aliyekuwa wa tatu Milioni 15.5.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KASEJA, DAMAYO, AZAM WANG'ARA TUZO ZA LIGI KUU 2012 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top