• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 27, 2012

  YANGA NA EXPRESS YA UGANDA JUMAMOSI TAIFA


  Yanga mazoezini ufukweni

  MABINGWA wa soka wa Afrika Mashariki na Kati, Young Africans Sports Club,siku ya jumamosi wanatarajia kujipima nguvu na Mabingwa wa Uganda timu ya Express  pambano litakalopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza na tovuti ya klabu  www.youngafricans.co.tz  Mratibu wa pambano hilo Frank Pangani amesema mipango ya mchezo huo tayari imekamilika ikiwemo Mabingwa hao wa Uganda Express inayotarajiwa kuwasili kesho jijini Dar es salaam wakitokea jijini mwanza ambapo mwisho wa wiki iliyopita ilicheza mchezo wa kirafiki mjini Shinyanga.
  Pangani amesema timu hiyo ya Express kutoka Uganda ambayo hivi karibuni ilicheza na Simba katika uwanja wa Kirumba inatarajiwa kuwa na msafara wa wachezaji na Viongozi jumla  26
  Timu hiyo ya Express kutoka nchini Uganda inarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam siku ya Alhamisi tayari kwa mchezo huo wa Jumamosi ikiwa chini ya kiongozi wa msafara Mohamed Katerega ambaye pia ni meneja wa timu hyo na msemaji wa timu ndugu Isack Mumena.
  Kwa upande wake Kocha msaidizi Fred Felix Minziro amesema kikosi chake kinaendelea vizuri na mazoezi  hivyo pambano hilo pia litasaidia kikosi chake kujiweka sawa kabla ya michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza Julai 14 Mwaka huu.
  Minziro amesema anafurahishwa na mazoezi yanayoendelea hivi sasa kutokana na bidii zinazofanywa na wachezaji wake ikilinganishwa na Mwaka jana anaamini kuwa michuano ya Kagame na ligi Kuu ya Vodacom itakapoanza  timu yake itafanya vizuri katika michuano hiyo.
  Kocha huyo amesema tayari ameona dalili za kila mchezaji kucheza kwa juhudi ili kuhakikisha kuwa kila mchezaji anapata namba za kudumu katika kikosi chake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA NA EXPRESS YA UGANDA JUMAMOSI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top