• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 28, 2012

  GAZZA SASA ANATIA HURUMA, INATAKA MOYO KUMTAZAMA


  Gazza

  UNAUMA UCHUNGU ... Gazza akiwa Dubai
  EXCLUSIVE
  Published: 27th June 2012

  GWIJI wa kandanda England, Paul Gascoigne yupo katika hali mbaya kiafya na kwa sasa amelazimika kuacha pombe na vilevi vyote ili kupambana na afya yake.

  Gazza alionekana ziarani nchini Dubai, akiwa katika kiti cha kusukumwa, ambaye hata kuzungumza ni tatizo.

  Kiungo huyo miongoni mwa wanasoka wa England waliobahatika kuwa vipaji hali ya juu, alihudhuria pati maalum aliyoalikwa Dubai.
  Gazza, mwenye umri wa miaka 45, akiwa kwenye kiti, sura yake ilionekana iliyopoteza matumaini na asiyeweza hata kuzungumza, zaidi mtu anayehitaji msaada.
  Pia amekonda ile mbaya, ambaye hajiwezi anasaidiwa tu na promota wake na rafiki yake wa siku nyingi, Jimmy Five Bellies.
  Gazza, ambaye amekuwa akishutumiwa kwa muda mrefu kwa uelvdi na utumiaji wa dawa za kulevya tangu anadheza soka, alikuwa Dubai katika ziara ya mazungumzo.
  Mwenyeji wake, Kareem Ghani alisema: “Ni janga namna hii. Alikuwa rafiki kweli, lakini sasa anaonekana kama mzimu.
  Gazza
  TABASAMU ...Nyota huyo akiwa amepozi kwa ajili ya picha na shabiki
  “Kila mtu karibu yake alikuwa anakunywa. Haya ni madhara ya ulevi. Hakika anahitaji msaa mapema, kabla muda haujawa umepotea.”
  Kareem, mwenye umri wa miaka 29, alisema: “Alikuwa nje ya hii. Alikuwa anacheza kamari kwenye meza na kupoteza, kwa sababu ni vigumu kumudu hiyo.
  Gazza
  HURUMA... Gazza kama anavyoonekana sura yake
  “Ni gwiji wa soka na hawezi kuishia kama hivi. Anahitaji ulinzi mzuri.”
  The Sun imeambiwa wiki hii kwamba Gazza alishiriki pati hiyo ambayo ni ya kupiga vita ulevi iliyoitwa “all you can drink” Euro 2012 party nchini Dubai, ikikitangaza kinywaji cha kuongeza nguvu, Red Bull.
  Gazza
  HALI TETE; Gwiji wa soka England katika kiti, mashabiki wakimtazama
  Nyota huyo ambaye hivi karibuni alitokea katika tangazo la vifaa vya michezo alipelekwa katika kituo cha tiba za uchizi, Mental Health Act mwaka 2008 na amekuwa akipambana na utumiaji wa dawa za kulevya aina cocaine, bulimia na bipolar disorder.
  Juzi usiku, Msemaji wa Gazza ALIKANUSHA alikuwa amelewa na ndio maana akarejeshwa rehab.
  Gazza
  NYOTA ... Mwaka 1991
  Wakala wake, Matt Jones alisema: “Paul Gascoigne kwa sasa yuko tu nyumbani Dorset baada ya wiki moja ya kuwa Newcastle na safari ya Dubai.
  “Anaangalia afrya yake tu na yuko vizuri — anatoka nje kila siku  — amekuwa akinywa tu vinywaji baridi na visivyo na kilevi.”
  Gazza
  Gazza ... katika bango
  Gazza
  SHUJAA... Gazza enzi zake uwanjani

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GAZZA SASA ANATIA HURUMA, INATAKA MOYO KUMTAZAMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top