• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 27, 2012

  MAN UNITED YAMPANDIA DAU WINGA TELEZA URENO


  Kocha wa Man U, Sir Alex Ferguson

  Gossip logo
  26 June 2012Last updated at 23:03 GMT

  Tetesi za J'tano magazeti ya Ulaya


  MAN UNITED YAONGEZA DAU

  KLABU ya Manchester United imezidi kukaza msuli katika jitihada zao za kumsajili winga wa Porto, James Rodriguez, mwenye umri wa miaka 20, baada ya dau lao la awali la pauni Milioni 30 kupigwa chini.
  KLABU ya Manchester City inaweza kutupa ndoana zake kwa beki wa pembeni wa Brazil, Dani Alves baada ya kutofautiana na uongozi wa Barcelona kwa kucheza mechi ya kirafiki bila ruhusa.
  KLABU ya Arsenal imejitoa kumpoteza Nahodha wake, Robin van Persie baada ya kukamilisha usajili wa pauni Milioni 13 wa mshambuliaji wa Ufaransa, Olivier Giroud kutoka Marseille ya Ufaransa.
  Rennes and France midfielder Yann M'Vila
  Yann M'Vila amekuwa akihusishwa na Arsenal
  NYOTA Branislav Ivanovic amemuambia kiungo wa Tottenham, Luka Modric ajiunge na Chelsea badala ya Manchester United au Real Madrid.
  KLABU ya Arsenal imepoza nia yake ya kumsajili kiungo wa Rennes, Yann M'Vila, mwenye umri wa miaka 21, baada ya kutofautiana na kocha wa Ufaransa, Laurent Blanc.
  KLABU ya Inter Milan ipo kwenye mazungumzo na Manchester City kwa ajili ya kumsajili kiungo wao hodari, Nigel de Jong.
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Brazil, Alexandre Pato, mwenye umri wa miaka 22, anaweza kuhamia Ligi Kuu ya England, mkataba wake utakapomalizika AC Milan mwaka 2014.
  KLABU ya Stoke City inataka kumsajili beki wa kati wa Houston Dynamo, Geoff Cameron, mwenye umri wa miaka 26, ahamishie makali yake England kutoka Ligi Kuu ya Marekani.

  EURO 2012

  KOCHA wa zamani wa England, Fabio Capello amtupia lawama mshambuliaji Wayne Rooney kwa kutolewa kwa England kwenye  Euro 2012, akisema kwamba mshambuliaji huyo anacheza vizuri akiwa na jezi ya Manchester United tu.
  Valencia and Spain full-back Jordi Alba
  Jordi Alba anatakiwa na Barcelona
  MSHAMBULIAJI wa Italia, Mario Balotelli yuko katika kejeli za kibaguzi kwa mara nyingine, baada ya gezi moja kumchapisha kama King Kong kuelekea mechi ya kesho ya Nusu Fainali Euro 2012 dhidi ya Ujerumani.
  BEKI wa pembeni wa Hispania na  Valencia, Jordi Alba, mwenye umri wa miaka 23, anatakiwa na Barcelona, Rais wa klabu hiyo ya Catalans, Sandro Rosell amethibitisha.
  KIUNGO wa Manchester City, David Silva amesema kwamba mchezaji mwenzao Andres Iniesta ni bora kuliko Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

  BENITEZ KUTUA SAMPDORIA

  KOCHA wa zamani wa Liverpool, Rafa Benitez yuko katika mazungumzo ya kuifunfisha Sampdoria.
  KOCHA Didier Deschamps ni miongoni mwa walimu wanaotajwa kuwamo katika orodha ya makocha wanaotakiwa na klabu ya Tottenham baada ya taarifa nchnini Ufaransa kusema kwamba anataka kuondokaMarseille. Full story: Daily Star 
  Norwich striker Grant Holt
  Norwich inamtaka Grant Holt
  KOCHA wa Norwich, Chris Hughton anafanya jitihada za kumbakisha katika klabu hiyo, mshambuliaji Grant Holt, mwenye umri wa miaka 31, baada ya kipa John Ruddy kusaini mkataba mpya wa miaka mine. Habari kamili: The Independent 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAMPANDIA DAU WINGA TELEZA URENO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top